gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,311
- 3,341
Siasa kwa upande wa wabunge wengi vijana wenye umachachari mkubwa kutoka Chadema wameonekana kua kimya sana mara tu Lowasa alipo hamia upinzani. Kwangu inanipa maswali mengi yasio na majibu hasa ninapotizama siasa za wabunge kama Mnyika,Lema na wengineo.
Mnyika alionesha utofauti mapema kabisa wakati wakumkaribisha Lowasa.Ilichukua muda kidogo kuonekana kundini hata watu wakaanza kuuliza humu mitandaoni wapi alipo Mbunge huyu machachari.Lakini hata baada yakujiunga kundini ile hamasa tunayoijua kwake haipo kabisa.Nasema hili kwani Mh Mnyika anafahamika vizuri juu ya uwezo wake wa ushawishi nakujenga hoja.
Imenilazimu kuhoji na kuhusianisha taswira hii na ujio wa Lowasa kwani kabla ya Lowasa kuhamia upinzani hii hali haikua kwa kiwango hiki.
Tizama mbunge kama Lisu kwa sasa ni ngumu sana kupata matukio yoyote kutoka kwake si mtandaoni,radioni ama Luningani.Ni nadra sana kupata taafifa zake.
Nahoji kwasababu natambua mchango wa wabunge hawa kwa Taifa.Natambua kelele zao hua zinafaida mkubwa kwa serikali.Na hii ndio dhana ya upinzani. Kwa sasa tunaona upinzani umepwaya kwa kiwango kikubwa kiasi ambacho inatia shaka chanzo ni nini. Mbunge pekee ambaye hajatetereka ni ZZK na natumai tutakubaliana sote katika hili.
Je ni ujio wa Lowasa ama Tanzania imepata raisi mchapakazi kiasi ya kwamba wabunge hawa wamekosa kabisa hoja?