Kuna la kujifunza toka CCM

Kuna la kujifunza toka CCM

Yakini

Member
Joined
Nov 20, 2012
Posts
75
Reaction score
19
Kuna la kujifunza kutoka CCM:
Kwanza niseme tu kuwa mimi naunga mkono upinzani, lakini nimeona kuandika uzi huu baada ya kuona kuna kitu ambacho sisi wapinzani tunachakujifunza toka kwa CCM. Pamoja na mapungufu mengi ya chama tawala lakini bado angalau wana mifumo ya kidemocrasia hata kama haijakamilika lakini kitendo cha kubadirisha viongozi wakuu kwenye chama ni kitu cha kuigwa. Hivi ndani ya vyama vyetu hakuna watu wengine wanaoweza kuongoza?? Kwamba lazima wawe ni wale wale tu. Lini Mbowe atapumzika, Lini Maalim Seif atapumzika, lini Mbatia atapumzika du, na isingekuwa mvutano pengine na Lipumba angekuwemo mpaka leo. Tunahitaji fikra mpya ndani ya vyama vya upinzani kama ni kweli tunahubiri democrasia. Inawezekana nikawa kinyume na wengi lakini, nimeona niwe muwazi kutoa maoni yangu.
 
Mimi ni CCM ila niwape angalizo tu kuongoza chama cha upinzani sio sawa na kuongoza chama tawala chenye rasilimali na kimedumu miaka zaidi ya 50. Vyama vya upinzani havina rasilimali na mkitaka vife anzeni mtindo wa kapokezana uongozi wa juu
 
Kwanza niambie hao viongozi wa upinzani Wako kikatiba au hawako kikatiba?, ccm toka ianzishwe haijawahi kufanya uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti ila huwa na mkutano wa kumthibitisha mwenyekiti tu
 
Mimi ni CCM ila niwape angalizo tu kuongoza chama cha upinzani sio sawa na kuongoza chama tawala chenye rasilimali na kimedumu miaka zaidi ya 50. Vyama vya upinzani havina rasilimali na mkitaka vife anzeni mtindo wa kapokezana uongozi wa juu
Maelezo yako hayagusi pia na waafrika kutaka kuwa na demokrasia kama ya wazungu.
 
Tunasikia mara kibao viongozi wa afrika kung'ang'ania madaraka na hadi kusababisha machafuko,na waafrika ndiye walewale tu hakuna waafrika wa chama tawala au upinzani.
 
CCM kwa miaka 50 imeongozwa na wenyeviti watano wakati CHADEMA kwa miaka 24 imeongozwa na wenyeviti watatu NCCR miaka 24 wenyeviti watatu,CUF wenyeviti watatu kwa hiyo si kweli kwamba vyama vya upinzani havibadilishi uongozi.
 
Tujifunze nini, matumizi mabaya ya fedha yasiyokuwa na sababu, watu zaidi ya 2000 kuitwa kubariki uamuzi ambao tayari uliishafanyika. kuturudisha enzi za kupiga kura mtu na kivuli, wangemkataa wangemchagua nani? tujifunze nini, tunauhakika gani kama hapakuwepo kura za hapana.
 
kila chama kina katiba na taratibu zake. ukitaka kufuata kijani wafanyavyo basi uwe ccm b au d
 
Tujifunze nini, matumizi mabaya ya fedha yasiyokuwa na sababu, watu zaidi ya 2000 kuitwa kubariki uamuzi ambao tayari uliishafanyika. kuturudisha enzi za kupiga kura mtu na kivuli, wangemkataa wangemchagua nani? tujifunze nini, tunauhakika gani kama hapakuwepo kura za hapana.
Hivi mwaka jana cdm ilimpataje mgombea urais wake!? Hapakuwa na wajumbe toka nchi nzima kuja kuitikia ndiooo.... Tena kwenye hotel la kifahari na mbwembwe zile zile zilizofanywa jana na ccm!!

Ukitaka kutoa kibanzi kwenye jicho la mwenzio anza na boriti lililo machoni kwako.
 
ivyo vyama bado ni vichanga
Kuna la kujifunza kutoka CCM:
Kwanza niseme tu kuwa mimi naunga mkono upinzani, lakini nimeona kuandika uzi huu baada ya kuona kuna kitu ambacho sisi wapinzani tunachakujifunza toka kwa CCM. Pamoja na mapungufu mengi ya chama tawala lakini bado angalau wana mifumo ya kidemocrasia hata kama haijakamilika lakini kitendo cha kubadirisha viongozi wakuu kwenye chama ni kitu cha kuigwa. Hivi ndani ya vyama vyetu hakuna watu wengine wanaoweza kuongoza?? Kwamba lazima wawe ni wale wale tu. Lini Mbowe atapumzika, Lini Maalim Seif atapumzika, lini Mbatia atapumzika du, na isingekuwa mvutano pengine na Lipumba angekuwemo mpaka leo. Tunahitaji fikra mpya ndani ya vyama vya upinzani kama ni kweli tunahubiri democrasia. Inawezekana nikawa kinyume na wengi lakini, nimeona niwe muwazi kutoa maoni yangu.
Ivyo vyama bado ni vichanga.Bado vinahitaji kiongozi wa namna hiyo.Vikija kushika madaraka vita badilisha tu viongozi.
ANC ya South Africa ilikuwa na viongoz wa juu wale wale kwa muda mrefu lakini baada ya kushinda uchaguz Mandela alikaa miaka mitano tu akastaafu.
 
Back
Top Bottom