ng'adi lawi
JF-Expert Member
- Sep 27, 2014
- 2,956
- 1,114
Kila siku kuna majengo makubwa ya kuishi na ya kibiashara yanajengwa. Pia kuna magari mengi ya kifahari yanaingia nchini. Serikali haijahoji vyanzo vya mapato haya labda kwa kutojua au kwa viongozi wengi kuwa wahusika. Ni wakati muafaka kufanya yafuatayo: 1. Majengo yote yafanyiwe tathmini na halmashauri za wilaya, miji na majiji kwa ajili ya kodi za majengo(property tax). Nakala za valuation reports zipelekwe TRA ili kuhakiki kama wenye hayo majengo wanalipa kodi ya mapato na kama mapato wanayolipia kodi yanalingana na thamani ya majengo hayo. Kama sivyo watozwe kodi ya 30% ya thamani ya majengo. Kama yamejengwa kwa mikopo ya benki mikataba isajiliwe TRA. Hapo serikali itapata kodi kutoka kwenye mapato ya ufisadi, ujambazi, madawa ya kulevya, uhujumu wa mali za umma na wafanyabiashara wakwepa kodi. Hakuna haja ya kuburuzana mahakamani kwa makosa ya zamani. Pia wakati magari yanaingia nchini kuwe na tax clearance certificate ili mapato ya kanunulia hayo magari yalipiwe kodi. Hii inafanyika katika nchi nyingi duniani kama Mauritius, India nk. Mhe Philip Mpango upo?