Uchaguzi 2020 Kuna kila dalili mwaka huu CCM inatoka madarakani

Ungesema tu kuwa kuanzia mchizi mitaani Hadi mawaziri the so called furaha imepungua
 
Mbona sasa unacheka cheka kama dada katongozwa halafu anataka hataki
Unajitetea Nini mkuu, we kubali umetoa boko uzi wako haufai, maana umedanganya umma. Jina lako linaendana na kile ulichoandikašŸ˜‚, Tila-lila hahahaha.
 
Tatizo si CCM kutoka madarakani,tatizo kubwa ni aina ya wapinzani wa kuiotoa CCM madarakani ndo tatizo,wapinzani hao bado hawapo na hawajatokea hadi sasa.
Tanzania kiujumla hakuna upinzani imara,upinzai uliobaki ni ule wa kutokea ndani ya CCM na ambao bado haujazaliwa hadi wakati huu.
Kuendelea kuwa na wapinzani wanaotumia upepo katika kuinyofoa CCM marakani ni kuendelea kuiacha CCM iongoze,CCM wao huwa hawatumii upepo wala tafiti za nje,wao wanafanya tafiti za ndani halafu nje wataenda kurekebisha wenyewe.
Wapinzani wao wanafanya tafiti za nje na kusahau kurekebisha ndani,unajua hii mbinu ni kama gari,ukitengeneza injini hata kama bodi likiwa bovu utafanikiwa safari,lakini ukitengeneza bodi wakati injini ni mbovu,safari yako haitofanikiwa,sasa sijui hapa wapinzani wanakwamia wapi.
 
Umepoteza muda mwingi sana kuandika lakini unaposoma katikati ya mistari utagundua kuna dalili za kuchanganyikiwa.Uliyondika ni kama umesimuliwa hadithi lakini akili haipo.
 
Hili na lo ni jibwa kama majibwa mengine.........ccm hatari kama tendo la ndoa...........
 
Sioni CCM kushindwa maana hao wapinzani wenyewe wanabaguana,kuna chama kimoja cha upinzani kinajiona kikubwa kuliko wengine ndio kishinde?Hao CCM unaosema wanamchukia mwenyekiti wao ni kwasababu kawabana sana ndani ya chama walikuwa wanakula tuu mali za chama sasa wamechukuliwa ulaji ndio chuki imeanzia hapo.Maana sasa hv chama kina hela ya kutosha kuliko kipindi chochote kile.
Bado CCM itashinda kwenye uchaguzi maana tume ya uchaguzi ni ile ile kumbuka mleta mada.
 
Mkuu,

sinauhakika kwa uliyoongea lakini hiki chama kutoka madarakan ndani ya miaka hii 100 sizani, labda tusubiri baada ya miaka Mia
Kujiamini kwingi, kunaweza kuleta msiba mkubwa.
KANU imebaki historia,haotasimama kamwe kuwa tena chama cha ukombozi Kenya.
CCM imesha fika ukingoni, kama haikuondoshwa kwa Kura itaondoshwa na washika Bunduki.
Wengi wameshachoka na Taarab za Kusifi Mnooo kusiko na tija kwa raia wa kawaida.
Time will Tell
 
Mimi nasema na narudia kusema ngoja mukinywee kikombe. Nakumbuka Kipindi cha Jakaya Kikwete mzee wa watu aliwaruhusu kila mtu awe mfalme katika eneo lake. Chadema akina Mnyika, Zitto na wengine wakapiga kelele serikali dhaifu na maneno kibao ya kejeri. Chadema wakasema Tanzania inahitaji Rais mkali asiecheka na watu. Tulieni Sasa sindano iwaingie maombi yenu yalifika yakasikika.
 
Huna kazi kuandika ujinga huu? Tukutane nov 2020 kama si Magufuli
 
Matokeo ya urais hayapingwi katika mahakama yoyote hapa Tz
 
Hivi ameshachukua fomu mtia nia mwingine au ni yule yule dikteta? Then wanasema kwao kuna demokrasia. Jamaa alistuka kuwa anaweza kukatwa kama mamvii
 
Hekaya za abunuwasi
 
Na kweli nadhani acha na ccm nao wakinywee kikombe!
Walidhani yataishia upinzani
Upinzani kwa sasa sio issue ni kama hawapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreā€¦