Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 57,754
- 92,178
Baada ya heka heka za kuwapata watumishi hewa, wakubwa walioruhusu upuuzi huo wamekuja na mbinu mpya ya kupinga uwepo wa watumishi hao kwa myindo wa pekee sana.
Mtindo huu ni kupunguza idadi hio ya Watumishi hewa ambapo utakua ni kati ya watumishi 50-100 kwa mkoa na 7-30 kwa Wilaya, idadi hii itaonekana ni reasonable na kwahio Jamaa hawa wenye deal lao hawatawajibishwa!
Kuna mtu aliwahi kuanzisha uzi hapa kuhusu watumishi hewa na niliweka wazi kuwa mkakati huo upo, na sasa mtasikia vyombo vya habari vikiripoti idadi ndogo sana maana wapigaji ni mtandao mrefu sana sana, na kwa taarifa yako pia watu hawa hutumia majina ya Wafanyakzi hewa hao kwenda kujichukulia mikopo kwenye Mabenki hasa NMB, kwa mfano kama ulishawahi kuwa Mwalimu na ukaondoka kwa sababu zozote zile kuna uwezekano mkubwa sana jina lako linatumika kumpatia mtu mwingine mkopo, wanafoiji kila kitu hadi signature yako.
Kwahio hii habari ya watumishi hewa ni pana na inahusisha hadi baadhi ya maofisa wa kwenye mabenki.