Mara ya kwanza kuna rafiki yangu aliibiwa sh.50000 kwa kuambiwa atume kwa mpesa kwa mfumo kama huu wa kwenye hizi shots, sasa hivi naona tena wamekuja hadi kwangu eti nichangie hela kama ionekanavyo hizi ni application za kupitia zoomtanzania.com
Mkuu naona tangu umeweka post yako haujapata michango yoyote ya wadau. Pengine hali hiyo imetokana na ukweli kwamba utapeli wa aina hiyo kwa wasaka ajira umeshajadiliwa sana hapa JF.
Hata huko Zoom Tanzania kwenyewe ulikotaja wameweka kabisa angalizo kwa watu kutokutuma fedha kwa taasisi yoyote inayotangaza nafasi za kazi kupitia mtandao wao.
Ilinitokea sema ilikuwa ni kampuni nyingine na kizuri siku mbili kabla kuna Aliyeanzisha uzi akitoa angalizo kuhusu hao watu na kama uzi ulivokuwa walituma vilevile.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.