Kuna haja ya kuwa na MA-DC na MA-RC?

chuwaalbert

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
3,598
2,115
Baada ya kuteua wakuu wa mikoa wiki chache zilizopita, Rais amewabadili kinyemela, wakuu wa mikoa ya Lindi na Shinyanga! wakati huo huo Nape Nauye, DC wa Masasi anasikika akiwa nje ya kituo chake cha kazi! Uwajibikaji hapa uko wapi? Anafanya kazi za CCM zaidi kuliko za serikali! Hii inaonesha kuwa kumbe hatuwahitaji Ma DC! Kuna haja ya kukomesha nafasi za wakuu za wilaya na wale wa mikoa kwani hazina TIJA kwa maendeleo ya Taifa!
 
jiulize hili jiji la daresalaam lina ma meya wanne na manaibu wao....

kuna faida gani????????
 
hoja yako ni nyepesi sana,kabla hujasema wasiwepo au wawepo tuambie majukumu yao na unazani wasipokuwepo atafanya nani.Nape asipokuwepo kituoni haimaanishi kuwa DC hayupo au DC maana yake physical appearance ya nape?
 
jiulize hili jiji la daresalaam lina ma meya wanne na manaibu wao....

kuna faida gani????????
tuangalie jambo hili kwa mapana,
meya ni mwakilishi wa nani?
mkuu wa wilaya ni mwakilishi wa nani?
lazima ujue nchi hii inawatumishi wa aina tatu
wanaqopigiwa kura
wanaoteuliwa kwa contract
wanaoajiliwa kama ajira ya kudumu,
kabla hujamhusisha meya ambaye ni sawa na mbunge jiulize majukumu yake ni yapi.
 
hoja yako ni nyepesi sana,kabla hujasema wasiwepo au wawepo tuambie majukumu yao na unazani wasipokuwepo atafanya nani.Nape asipokuwepo kituoni haimaanishi kuwa DC hayupo au DC maana yake physical appearance ya nape?

Lakini mkuu hapo kuna ukweli fulani wala jamaa tusimbishie kwa ushabiki tu!

Ukifanya kazi karibu na hawa watu "DC na DED" unaona kabisa hapakuwa na haja ya kuwa na DC. Unaenda pale kuulizia habari ya maendeleo anakuelekeza kwa DED au kwenye kikao lazima DED awepo, vinginevyo mambo mengi DC anakuwa hayafahamu kwa undani. Hawa jamaa wako pale kisiasa zaidi, hasa hasa kulinda maslahi ya chama cha magamba! Au na wewe Kanyasu unanyemelea u-DC nini?


Ukiangalia JDs za ma-DCs utaona kabisa kwamba hayo majukumu yao yangeweza kusambazwa na kutekelezwa na DED na hivyo ingetupunguzia mzigo wa kuwa na matumizi yasiyokuwa ya lazima. Nchi yetu vyeo ni vingi mno jamani, kwa nini isingetafutwa namna ya kupunguza gharama? (DED, DC, DAS, RC, RAS, n.k.), yaani hawa wote ukiwakuta wanavyoingiliana kwenye majukumu ni mkanganyiko siyo kidogo.
 
Back
Top Bottom