Kuna haja ya kuitambua hii 'misemo' ya Mbwiga?

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Nimekuwa nikimsikia mara kwa mara mmoja wa Mwana redio anayeitwa au kujiita Mbwiga, huyu bwana amekuwa na misemo tofauti tofauti kila anapopata nafasi ya kuzungumza redioni.

Na mingi ya hiyo naona huwa inabeba maana iwapo utaitafakari...kwa mfano jana usiku nikamsikia akisema "ukimuona Ngedere barazani basi hakuna fugo la Mbwa. kama kuna Mbwa Ngedere atashinda juu ya Mkorosho", Pia tena akasema "Tetere hata umpende vipi ukimtoa bandani atatoroka tu" sijui kama nimepatia kikamilifu alivyotamka ila hivyo ndivyo ninavyokumbuka na nilivyomuelewa.

Iwe anatunga yeye au anarejea tu misemo iliyopo bado naona anafanya kazi kubwa ya kuikumbusha jamii hiyo misemo...naona ana mchango kwenye kuisisimua lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

Bila kusahau baadhi ya maneno yaliyoingia kwenye matumizi kutoka kwake, maneno kama "figisu" n.k.
 
Figisu figisu,,Unatiatia huruma kaa stand ya baiskeli,Msimu wa maembe nyani hakondi,Asiye na macho abandike goroli,
 
Back
Top Bottom