Kuna faida kubwa kwa mwanamke watoto wake wote kuwa na baba mmoja

Kuna faida kubwa kwa mwanamke watoto wake wote kuwa na baba mmoja

Holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
6,725
Reaction score
13,747
Wakuu,
Namshukuru sana Mungu kwa kumfanya mama awe na moyo wa uvumilivu mpaka ameacha kuzaa sisi watoto wake wote ni wa baba mmoja.

hii ni nzuri sana inasababisha kutokuwepo kwa mgogoro na migongano ya kimasilahi baina yetu kwani hakuna mtu ambaye ni wa baba tofauti

kuwa na watoto wa baba tofauti tofauti huleta utofauti wa tabia baina ya watoto mwingine ni mwizi,malaya au mchoyo kutokana kurithi kutoka kwa baba zao,hivyo ukiwa na watoto wa baba mmoja basi hakuna huo utofauti huo wa tabia za kurithi kutoka kwa baba zao.

kuwa na watoto wa baba mmoja huleta furaha ndani ya familia kwani mtakuwa mko pamoja mnajuana na kufahamiana,tofauti na kuwa na watoto wa baba tofautitofauti kwani mwingine ataenda na baba yake mwingine huku mwingine kule hivyo kupotea kwa ukoo huwa ni rahsi sana

niwasihi dada zangu ambao bado hamjawa ma single maza tafuteni wanaume ambao mnaamini watakuwa ma maisha yenu yote,hata kama unapitia changamoto gani katika ndoa jitahidi kuvumilia.

Ni hayo machache ndugu zangu
 
Ni vizuri sana mkizaliwa wote baba mmoja lakini tabia kama wizi, uchoyo n.k hazipo tu kwa watoto waliozaliwa baba tofauti mnaweza kuzaliwa wote sehemu moja na miongoni mwenu akatokea mwizi na mchoyo vile vile.

Hata furaha ndani ya familia haipo kwa waliozaliwa na baba mmoja tu, kuna familia haziishi migogoro kila leo na wote wamezaliwa sehemu moja.

Familia ni zaidi ya kuzaliwa tumbo moja. Kuna watu wamezaliwa tumbo moja na mmoja akifariki hawazikani.
 
kuna tabia/hali otomatiki ni za kurithi kutoka kwa wazazi. Usikatae
 
Na wangekuwa wa baba mmoja na mama mmoja wanatabia za umalay,wizi,utapeli,roho za ajabu ungefanyeje
 
kuna tabia/hali otomatiki ni za kurithi kutoka kwa wazazi. Usikatae
Mkuu sipingi hoja yako, ndio maana nilianza kwa kusema ni vizuri kama watoto wote mkizaliwa sehemu moja ila hoja yangu ni kwamba tabia mbaya za watoto hazitokani na watoto kuzaliwa baba / mama tofauti.

Mfano mko watatu, mmezaliwa baba mmoja mama mmoja, baba tabia zake mchoyo sana mama tabia yake roho mbaya sana, je miongoni mwenu hatotokea mtoto mwenye tabia za mama au baba?
 
Ni
Sisi tunazaa ovyo au nyie ndo mnamwaga kiholela?
[/QUOTE]
Kumwaga kiholela hata chini tunamwaga, ila kuzaa kiholela hadi umwagiwe ndani na mtu yeyote bila hata kuchagua. Huko ndo kuzaa kiholela.
 
Back
Top Bottom