Kuna dirisha la Mabadilko

Kuna dirisha la Mabadilko

Toosweet

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2012
Posts
2,140
Reaction score
1,983
Kwenu Tanzania,

Pole ni kwa kuondokewa na kiongozi wa nchi. Kiongozi mkuu wa nchi anapoondoka,iwe kwa kumaliza muhula au kwa kufa,lazima kuwe na mabadiliko ya watendaji, mtazamo mpya, mtindo wa uwajibikaji, Uhuru wa mawazo au ugumu wa kutoa maoni nk.

Kuna kisa cha zamani kinachohusu mzee aliyekuwa na akili na hekima na aliyekuwa na jibu kila alipoulizwa swali. Watoto wawili wakaidi waliazimia kumkomesha. Walikamata panzi na kumfumba kwenye kiganja kisha wakamwendea na kumwuliza, haya babu, tuambie, panzi aliye kwenye kiganja ni mzima au amekufa? Walipanga akisema amekufa tu, yule aliyemficha kiganja ni angemwachia kwa kuwa hakumbana na panzi angeruka na kuondoka. Akisema yuko hai, angeminywa na kufa kisha kudondoshwa chini Babu angeumbika.

Mzee yule aliwaangalia na kusoma janja yao. Aliwaambia,"Uhai au uzima wa panzi aliye mkononi unategemea na aliyemkamata anaamua hatima yake, si Mimi".Watoto wakaumbuka.

Hatima ya Tanzania baada ya Magufuli kuondoka haiko mikononi mwa CCM, CHADEMA, ACT Wazalendo, CUF au chama kingine chochote. Hatima ya Tanzania iko mikononi mwa Watanzania wote. Hakuna mtu binafsi mwenye hatima ya wananchi wote, kwamba kama hayupo basi jahazi linazama. Hivi ndivyo wengine, hasa whafidhina wanavyotaka tuamini.

Inawezekana hayati Magufuli alifanikiwa kutekeleza majukumu yake almost single handedly.Taasisi zimebaki kama watazamaji,hakuna urasimu wala kuchelewesha mambo. Toa amri, mambo yanaenda fasta. Watanzania wengine walijimilikisha rais, hawakutaka wasio wa chama chake wamkosoe.Wakae kimya kwa kuwa hawakushinda uchaguzi. Wamuache Chuma achape kazi.

Political exclusion imeleta ubaguzi.Hata tukitangaza mafanikio kwenye kipindi cha maombolezo lakini ukweli utabaki kuwa nchi imegawanyika na inahitaji mabadiliko. Wakosoaji wameipata joto ya jiwe. Hata wakati huu wa maombolezo kuna wanaosema, haya sasa amekufa, furahini basi. Nao hujibu, haya, kiko wapi, tuone sasa.

Udhaifu wa CCM ulisababisha Magufuli afanye kazi peke yake bila checks and balances.Walichekelea wapinzanii wao walipokong'otwa na kuona hakuna haja ya upinzani.Wamefanya dhambi kubwa sana. Huwezi kuleta maendeleo ya kweli kwa kubagua wengine. Maendeleo ni jambo la pamoja ni jambo shirikishi linalohitaji mchango toka mawazo tofauti na si mawazo ya upande mmoja.

Dhambi nyingine mbaya tuliyofanya ni kujitenga na dunia. Kukataa yote ambayo wengine wanafanya na kujidai sisi ni wazalendo zaidi.Tulichokipata tunakijua. Tupokee mawazo ya wengine na kuyafanyia kazi. Watanzania, tusiwaachie viongozi pekee kuamua hatima yetu. Tuhusike wote kusaidia viongozi ili wasiwe miungu isiyohojika. Lazima tuwe na mabadiliko ya kushiriki wote kwenye kujenga nchi yetu. Tukatae ubaguzi na kutaka kuwa juu ya wengine. Tusikwepe wajibu kama wale watoto watukutu wakati hatima yanchi iko mikononi mwetu.

Mheshimiwa rais, mama Samia aepuke watu wanaojidai ni wazalendo zaidi kuliko wenzao na kutaka kudumisha mila.Lazima tuwe na mabadiliko ili tusonge mbele kwa kuwa ni enzi mpya.
Mungu ibariki Tanzania.
Nawasilisha.
TS
 
Back
Top Bottom