Urio kimiroI
Senior Member
- Jan 2, 2016
- 146
- 74
[HASHTAG]#KAULI[/HASHTAG] ZA wenye KAULI
JE, KUNA MKAKATI WA SIRI KUHUSU UFAULU WA WANAFUNZI SHULE ZA BINAFSI?
Kwa muda mrefu sasa shule za sekondari za binafsi nchini Tanzania zimeendelea kushika nafasi za juu katika mitihani mbalimbali inayoongozwa na baraza la mitihani la Taifa, NECTA.
NECTA ni baraza la taifa la mitihani lilioanzishwa kwa mujibu wa sheria ya bunge ili kuratibu na kusimamia uandaaji na usahihishaji wa mitihani kama moja ya kazi zao.
Matokeo yote ya mitihani katika shule za sekondari na shule za msingi hutangazwa na baraza hili baada ya kujiridhisha kwamba, matokeo ni halali kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za mitihani.
Miaka ya nyuma shule za serikali ndiyo zilikuwa vinara na KIDEDEA katika kuongoza ufaulu wa wananfunzi kwa darasa la saba, kidato cha Nne na kidato cha Sita. Pamoja na kwamba mazingira ya sasa hivi ni mabovu katika shule nyingi za zamani hasa zile zilizokuwa na JINA LA SHULE ZA VIPAJI MAALUMU.
Kuna mkakati wa siri kati ya baadhi ya wamiliki wa shule binafsi na suala la ufaulu wenye 'mashaka makubwa'.
Mkakati huu unahusisha baadhi ya wanasiasa ambao ni ama ni wamiliki kamili au wanahisa katika makampuni yanayomiliki shule binafsi, baadhi ya wanasiasa ambao wapo katika kazi maalumu ya kuishinikiza serikali kubadili mifumo mbalimbali katika sekta ya elimu, kwa maslahi yao binafsi, wakuu wa shule binafsi, wamiliki wa shule binafsi, na baadhi ya matumishi wasio waaminifu wa baraza la mitihani la Taifa, NECTA.
Mkakati huu umewekwa kwa lengo la kuhakikisha baadhi ya shule binafsi zinashika nafasi husika ili kuvutia mazingira mazuri ya kibiashara.
Baadhi ya mambo yaliyomo katika mkakati huu, ni pamoja na kuwafundisha wanafunzi sehemu za maswali ya mitihani ya vitendo(wanafunzi hufundishwa mitihani bila wao kufahamu), Practicals nyingi katika baadhi ya shule za sekondari hutolewa mapema na kufundishwa kwa wananfunzi katika namna maalumu ili kumfanya mwanafunzi akiingia kwenye mtihani anakutana na maswali kama yalivyo.
Mmoja wa walimu ambaye amejitaja kwa jina moja la Joseph, anayefundisha moja ya shule iliyopo katika kumi bora amesema, "mikakati ni mingi sana mpaka mwanafunzi afaulu ndugu, lakini moja wapo ni kuwafundisha mitihani wanafunzi hasa Practical''.
Mwalimu Joseph ni miongoni mwa walimu wanaopinga mchezo huo katika shule hiyo na hata kufikia kutishiwa kufukuzwa kazi katika shule hiyo ambayo inamilikiwa na mmoja wa wanasiasa wakubwa hapa Tanzania.
"Tumekuwa tukilalamika kwanini tusiwaache wanafunzi wanafunzi wajipime kama tunavyofanya katika mazoezi ya kawaida lakini tunonekana ni wasaliti, nakuhakikishia kwamba hata hizo kumi bora ndiyo maana wengi wao wakiingia vyuoni wanaishia kuwa wa mwisho".
Mmoja wa wanafunzi Husna Hamisi wa shule moja ya Jijini Dar Es Salaam, aliyemaliza kidato cha Nne mwaka 2015, anasema anashukuru Mungu kwamba karibu yote waliyofundishwa hasa Practicals, waliyakuta na hivyo hii ilimsaidia kufaulu masomo yake.
Mwalimu Zuwena Kabanga, mkoani Morogoro anasema, ''mara nyingi sisi huwa tunaandaa mitaihani ili kuwasaidia wanafunzi wetu wafaulu zaidi, na moja ya mbinu zetu ni kuwapa exposure mapema bila wao kufahamu''. Alipoulizwa kwanini anafanya hivyo alijibu bila woga kwamba huwa wanafanya hivyo ni sehemu ya utaratibu wao, na yeye ameukuta upo.
''Baadhi ya walimu huwa na mawasiliano ya moja kwa moja na waandaaji wa mitihani ya NECTA wasio waaminifu, na hivyo huwapa taarifa muhimu kuhusu nini kitakuwepo katika mitihani hiyo na hivyo hii huwasaidia kuweka mkakati maalumu wa ufundishaji, hasa kwa wanafunzi ambao wanakuwa mwaka wa mwisho.'' Ameeleza mmoja wa walimu wakuu mstaafu kutoka shule moja wapo ya serikali.
''Sisi hatuwezi kufanya hivyo huku serikalini, kwa sababu ni mpango unaohusisha watu wenye fedha nyingi, na baadhi ya wanasiasa'' . Ameongeza mwalimu huyo mstaafu.
Badala ya watu kuzilaumu tu shule za serikali kutofaulisha na kuzisifia shule za binafsi kwa kufaulu wajiulize maswali haya.
Nani yuko nyuma ya umafia huu wa elimu(Ni nani akina MASTERMIND wa mikakati hii ambayo inaligawa taifa)?
Kwanini shule za vipaji maalumu zimekufa? au ni kwa sababu serikali imeshindwa kabisa katika usimamizi?
Je, Baraza la mitihani la Taifa NECTA, limezungukwa na kina nani , hasa katika utunzi wa sera na je mazingira ya mitihani yakoje katika namna ambayo hutolewa kwa watahiniwa?
Kwanini Dr Ndalichako aliondolewa barala za mitihani? Kwanini rais John Pombe Magufuli amemrudisha kwa kumpa mamlaka makubwa?
Je, ni utafiti gani umewahi kufanywa na taasisi yoyote kubainisha uhusiano uliopo kati ya wamiliki wa shule binafsi na NECTA.
Je, Taasisi ya HakiElimu haiyajui haya?
Mwisho kabisa tujiulize ni nini nafasi ya vyombo vya habari katika kuchunguza, kubaini na kuripoti UMAFIA huu ambao kwa sasa umeingia katika vichwa vya waliowengi kwamba hakuna namna tena nchi yetu imeshindwa kurudisha heshima ya shule za serikali?
Jadili kwa hoja.