Mukuru
Member
- Apr 14, 2009
- 40
- 0
Kwa mazingira ya kisiasa ya sasa nchini ni kujidanganya kuwa kiongozi wa upinzani anaweza kuwa Rais kupitia njia ya kura. Kwa hiyo yeyote aliyetarajia kuwa Dr. Slaa angekuwa Rais ama hayafahamu vizuri mazingira halisi ya kisiasa au anajidanganya kwa kujipa matumaini 'hewa'. Haiwezekani kuwa Rais nje ya CCM kwa mazingira ya sasa kwa sababu nyingi tu - nitaorodhesha chache:
- CCM inatumia rasilimali 'zake' na za nchi kuhakikisha mgombea wake anakuwa 'celebrity' na hivyo kuwazuga wapiga kura wengi hasa wa vijijini.
- Tume ya uchaguzi inaundwa na mwenyekiti wa CCM - hivyo wajumbe wake lazima watalinda 'ulaji' wao. Hawawezi kuhatarisha 'ajira' yao kwa kuzingatia haki.
- Katiba imeionyoonyeshea njia CCM kwani inatamka wazi kuwa NEC ikishatangaza matokeo ya urais, hakuna mahakama yoyote inayoweza kuhoji matokeo hayo.
- Bado Dr. Silaa anahitaji walau kipindi kingine kuweza kuwashawishi watanzania hasa wa vijijini umuhimu wa mabadiliko. Inachukua muda kwa walio wengi kuelewa hasa ukizingatia tumekuwa katika mfumo wa chama kimoja kwa muda mrefu.
- CCM inatumia mtaji wa umaskini na elimu duni kwa wa watanzania walio wengi. Ukiwa maskini wa hali na elimu, uwezo wako wa kuangalia mbali unapungua, hivyo faraja ya muda mfupi ni kitu kikubwa bila kuangalia athari hasi za muda mrefu. Hivyo CCM hutumia vitu kama tisheti, kofia, vitambaa na vijisenti kama kivutio kwa wapiga kura. Kwa mwananchi ambaye hata uwezo wa kununua aspirini 2 hana, kitu kama kofia ni kitu cha thamani kubwa kwake.