mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
JK aliamini katika Kutoka kutafuta fursa kwa wananchi wake, Watu wengi nikiwemo na mimi tulipinga tulipoona zinazidi.Kuthibitisha hilo JF ulianzishwa uzi wa kuratibu safari za Rais na wengine walienda mbali hadi kupiga hesabu ya gharama. Mfano Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005. Na hapa Tusimseme mkuu wetu tu wabunge ndio walikuwa wanapishana airport kila kukicha. Kuna wakati baadhi waliwahi kwenda hadi Ethiopia kuangalia ufugaji wa kuku wakati hapa bongo kuna wafugaji wakubwa na wanafanya vyema. Kuna wakati tulisikia wengine walipishana kauli wakiwa ughaibuni. Hapa sijazungumzia watumishi wa umma nao walisafiri sana.
Sisi kama wananchi ambao imani Zetu zimejengwa kwa Wanasiasa, Tulipinga safari tukiongozwa na wanasiasa wachache. Wengine Tuliziunga mkono ili tusionekane waovu na wasaliti wa mipango ya ilani na rais.
Miaka 10 ikapita, Kaja kiongozi mwingine JPM, kaona sasa imetosha, Tuangalie safari za miaka 10 tumejifunza nini , Tuangalie Fursa za kutekeleza tuliyojifunza huko Ughaibuni. Sasa Ikiwezekana Wao ndio waje kututembelea Tutawaalika ikiwezekana.
Mlinganyo Umegeuka sasa Watanzania Tuliokuwa Tunapinga Safari za nje, Tunaponda kutokwenda nje kwa watumishi na Rais, Tunasema wao wanaokuja hawanafaida ni upotevu wa pesa. Wale Tuliokuwa Tunashabikia na kusheherekea kwa misingi ya kutetea serikali awamu ile leo tunapinga na kupongeza zoezi la watumishi kutokwenda nje hata kama ni wahanga.
FUNZO LA KWA NINI TULIPASWA KWENDA UGHAIBUNI WAKATI ULE WA JK NA SIO SASA.
Kiongozi shupavu wa Kijapani IWAKURA TOMOMI, mWAKA 1871 alitengua katazo la wajapani kutoka nje ya nchi yao. Yeye akiwa kiongozi wa msafara aliondoka na viongozi wenzake pamoja na wasomi wake zaidi ya 52 ndani ya meli wakielekea Ulaya wakatua LIVERPOL na Marekani wakifikia SAN FRANSCISCO Kujifunza Maendeleo. Mission ilikuwa ni Moja na Baada ya hapo ni Utekelezaji hakuna longolongo. Safari hii ndio sababu ya Japani kuwa nchi ya kwanza kuendelea far east.
Waliporudi Japani Ilipata nguvu kubwa na kutawala eneo lote kwa mkono wa chuma Sio CHINA wala KOREA wote walikaa chini ya kisiwa kidogo sana kiuchumi,kijeshi na kimaendeleo.
JK kamaliza hiyo kazi sasa JPM afanye utekelezaji Watanzania Tumebadilika tena hasi wamekuwa chanya waliokuwa chanya wamekuwa hasi.
KUMUELEWA MTANZANIA, INAHITAJI AKILI YA ZIADA,