WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 947
Donald Trump aliingia ofisini akiahidi kubadilisha sura ya siasa za Marekani na kurejesha madaraka kwa raia.
Kufikia sasa, amefanikiwa kufanya nini? Tunafuatilia maendeleo ya rais kwenye ajenda zake na jinsi zinavyopokelewa na watu nchini Marekani.
Ni hatua zipi kuu ambazo Trump ametekeleza?
Njia moja ambayo Trump anaweza kutekeleza madaraka yake ya kisiasa ni kupitia kwa amri kuu, ambayo haihitaji kuidhinishwa na bunge.
Hakutupa muda katika kutumia madaraka hayo ikiwemo kujiondoa kutoka kwa makubaliano ya biashara ya nchi za Parifiki, Trans-Pacific Partnership (TPP) na kuendelea na ujenzi wa mabomba mawili ya kusafirisha mafuta yanayokumbwa na utata.
Huku akionekana kutumia madaraka yake kwa njia ya haraka, aliweka sahihi idadi sawa na amri alizoweka sahihi mtangulizi wake Barack Obama, wakati wa majuma ya kwanza ofisini, lakini hata hivyo Trump amempiku Obama.
Baadhi ya amri kuu za Trump zina lengo la kutimiza ahadi zake wakati wa kampeni, lakini ushawishi wake ni mdogo.
Huku amri kuu zikiwa na uwezo kubadilisha jinsi mashirika ya serikali yanatumia fedha, amri hizo haziwezi kuyapa mashirika hayo fedha au kuyawekea sheria mpya.
Madaraka hayo yote ni ya Bunge la Congresss.
Kwa mfano amri ya kwanza ya Trump ilikuwa ni ya kupunguza nguvu za Sheria ya Bima Nafuu ya Afya, ambayo hufahamika kama Obamacare, lakini ahadi yake ya kuibadilisha itahitaji kuidhinishwa na Congress kwa sababu inahitaji sheria mpya.
Viwango vya umaarufu wake ni vipi?
Wakati Trump aliapishwa tarehe 20 mwezi Januari, alikuwa na umaarufu mdogo kuliko rais yeyote aliyewahi kuapishwa Marekani.
Alitaja takwimu hizo kuwa za uongo, lakini upinzani aliokabiliana nao ulionekana wakati maelfu ya watu waliingia barabarani siku moja baada ya kuapishwa kwake.
Marais wengi huingia ofisini wakiwa na umaarufu mkubwa.
Marais George Bush na Barck Obama walikuwa na umaarufu wa karibu asilimia 60 ilipofika mwezi wa nne, Trump alikuwa na asilimia 40.
Trump amechukua hatua za kupunguza uhamiaji haramu?
Uhamiaji ilikuwa ajenda kuu ya Trump wakati wa kampeni na ametia sahihi amri kadha kuu zenye lengo la kutekeleza ahadi zake.
Moja ya amri zake ni kuwa Marekani itajenga ukuta kwenye mpaka wake na Mexico ambapo ua wa maili 650 tayari umewekwa.
Lakini Trump anahitaji idhini ya Bunge la Congress ya ufadhili kabla ya ujenzi huo kuanza. Anasisitiza kuwa gharama ya ujenzi huo italipwa na Mexico licha ya viongozi wake kupinga.
Tamko la Rais la kuwatimua wahamiaji haramu linaonekana kama jambo rahisi lakini kuna ushahidi kuonyesha kuwa hilo ni kinyume.
Kati ya mwaka 2009-15 utawala wa Obama uliwafukuza watu milioni 2.5 ambao wengi walikuwa wamepatikana na hatia ya kutenda uhalifu
Lakini bado kuna wahamiaji milioni 11 wasio na vibali vya kuishi nchini Marekani, wengi kutoka Mexico.
Idara za uhamiaji zimeendesha msako kote nchini tangu Trump achaguliwe lakini ni vigumu kusema hatua ya kuwakamata na kuwafukuza imeongezeka.
Uchumi unafanya vipi chini ya Trump?
Wakati Barack Obama alichaguliwa kama rais mwaka 2009, Marekani ilikuwa imekumbwa na hali ngumu ya uchumi kuwahi kushuhudiwa tangu miaka ya 1930, huku watu 800,000 wakipoteza ajira mwezi wake wa kwanza.
Lakini baadaye mwaka huo Marekani ilifanikiwa kubuni nafasi nyingi za ajira.
Kwa jumla ajira milioni 11.3 zilibuniwa chini ya uongozi wa Rais Obama.
Trump amepinga takwimu hizo na baada ya kuapishwa aliutaja uchumi kuwa mbaya.
Wakati wa ripoti ya kila mwezi iliyotolewa mwezi Machi ikionyesha kuwa ajira 235,000 zaidi zilibuniwa mwezi Februari, mkuu wa mawasiliano katika ikulu ya White House alisema kuwa hizo ni habari njema kwa wafanyakazi wa Marekani.
Wakati wa kampeni Bwana Trump aliapa kubuni ajira milioni 25 katika kipindi cha miaka 10.
Aliilaumu Mexico na China kwa kuiba mamilioni ya ajira na kuapa kurejesha ajira hizo nyumbani.
Bima ya afya imekuwaje?
Mpango wa bima ya afya ungekuwa kipimo cha Trump baada ya kuutumia sana katika kampeni yake.
Mpango rahisi wa Rais Obama ulisaidia zaidi ya watu milioni 20. Lakini Trump alisema kuwa angeufanyia marekebisho mara moja.
Warepublican walizindua mpango wao mwanzoni mwa mwezi Machi.
Rais Trump aliunga mkono mpango huo lakini ulikaguliwa vikali na ofisi ya bajeti ya Congress, shirika la serikali lisiloegemea upande wowote, lilisema kuwa utasababisha watu milioni 24 zaidi kukosa bima ya afya ifikapo mwaka 2026.
Wanarepublican walikuwa wameahidi mpango mpya wa bima ya afya baada ya likizo ya Pasaka lakini bado haijulikani una nini, au kama chama cha Republican kitauunga mkono na ikiwa utapata kura zinazohitajika kuweza kupitishwa na Bunge na hatimaye kuwa sheria.