a sinner saved by Christ
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 1,966
- 2,200
Yohane 14:15-20
“Mkinipenda mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba naye atawapeni Msaidizi mwingine, atakayekaa nanyi milele. Yeye ni Roho wa ukweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea kwa sababu hauwezi kumwona wala kumjua. Lakini nyinyi mnamjua kwa sababu anabaki nanyi na yu ndani yenu.
Yn 14:23
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
KUSHIKA AMRI ZA MUNGU.
ambazo kubwa ni mbili
1)kumpenda MUNGU
2)kumpenda WATU wote.
katika kupenda watu wote
utakuwa na amani na watu wote hutakuwa na adui,na kama una adui yako utampenda na kuwa na amani naye ni sawa na kusema hutakuwa na uadui na mtu, hutakuwa na kinyongo,hutabeba watu moyoni,utasamehe watu bila kuchoka,hutasengenya,hutakuwa mchoyo,hutaiba,hutatamani mali ya jirani yako,hutaiba ,huta UA kuua kuna anzia moyoni ukishamchukia mtu ukawa na kinyongo naye unaweza ukawa tayari moyoni mwako umeshamu ua tayari katika mawazo yako moyoni, utakuwa na huruma kwa wengine ,hasa masikini wanyonge wajane ,wahitaji,wafungwa,wagonjwa n.k,hutatamani mke wa jirani yako wala mali yake..
UPENDO NI UTAKATIFU,mana Mungu ni mtakatifu na Mungu ni Pendo.
Ukiwa na amani na watu wote na upendo na watu wote hata maadui zako,ukawa na moyo safi wa kuachilia msamaha kutokuwabeba nankuhifadhi chuki na maumivu moyoni na vinyongo na watu..unakuwa kama matakatifu fulani hivi na huo utakatifu ndio tunaotakiwa kuwa nao.
30 Katika kujibu swali hili, Yesu akasema, “Mtu mmoja alikuwa anasafiri kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Akiwa njiani alivamiwa na majambazi, wakamchania nguo na kumpiga. Kisha wakamwacha amelala chini akiwa katika hali ya kufa.
31 Ikatokea kuwa kuhani mmoja alikuwa anasafiri kupitia njia hiyo hiyo. Alipomwona, hakusimama ili amsaidie, alikwenda zake. 32 Kisha Mlawi[a] alipokaribia na kumwona yule mtu, alipita upande mwingine. Hakusimama ili amsaidie, Alikwenda zake.
33 Ndipo Msamaria mmoja aliyekuwa anasafiri kupitia njia ile ile, alipofika mahali ambapo mtu aliyejeruhiwa alikuwa amelala, alipomwona alimhurumia. 34 Alimkaribia ili amsaidie, akamsafisha majeraha kwa mafuta ya zeituni na divai,[c] kisha akayafunga majeraha yake. Msamaria alikuwa na punda. Akampandisha juu ya punda wake na kumpeleka mpaka kwenye nyumba ya wageni. Akamhudumia huko. 35 Siku iliyofuata, Msamaria alitoa sarafu mbili za fedha na kumpa mtunza nyumba ya wageni, akamwambia, ‘Mtunze mtu huyu aliyejeruhiwa. Ukitumia pesa nyingi zaidi kwa kumhudumia, nitakulipa nitakapokuja tena.
UTAJUAJE KAMA UMELIPOKEA NENO?
Zakayo mtoza ushuru alipomuona YESU ambaye ndio NENO alibadilika kuanzia miyoni,rohoni mpaka nje mwilini au matendo yake ,akaanza kuwagawia watu mali zake na wote aliowaibia akaanza kuwarudishia mali zao alizowadhulumu NENO lilimwingia moyoni mwake akafunguka moyoni akaona alitenda dhambi hakutenda kwa haki wala hakutenda kwa upendo na huruma.Yani mpaka watu wakamtambua kuwa huyu amebadilika amekuwa mpya siyo yule zakayo mtoza ushuru wa mwanzo.
KUJUA SANA MAANDIKO kuwa na elimu kubwa ya dini kufahamu maandiko au kuwa kuhani au mlawi au kiongozi wa kiroho/ dini inaweza isitusaidie kulitenda neno
" can you practice what you preach"
kuyaishi yale tuliyoya amini..na kuyahibiri IMANI iendane na matendo mema,kama msamaria mwema alivyotenda.
imani bila matendo imekufa.
Katika kushika NENO la Mungu.
kwa mfano wa huu alioutoa Yesu juu ya mtu aliyejeruhiwa na kuachwa barabarani na majeraha yake.
akapita KUHANI hawa ni watu wenye elimu ya dini na maandiko,kadhalika MLAWI hawa ni watu wenye kuijua dini na wanatumika kama viongozi wa dini wasomi wenye elimu ya dini na maandiko ya torati .
lakini hawajalishika NENO la Mungu moyoni mwao yani katika kuliishi na kulitenda katika maisha yao.SHIKA NENO TENDA NENO.
ndio maana unaona wameshindwa kuonyesha upendo kwa majeruhi aliyetelekezwa barabarani akiwa na majeraha ,wakampita pembeni.
Usipompenda jirani yako unayemuona hata huwezi kumpenda Mungu usiyemuona.ni sawa na kusema wewe humpendi Mungu mana hujashika amri yake kuu aliyoagiza tupende watu wote hata maadui zetu,tuwaombee wanaotuudhi,tuwaombee maadui,tutafute kuwa na amani nao.
Hata unapokwenda kutoa sadaka madhabahuni kabla hujaweka katika madhabahu au chombo cha sadaka ukikumbuka una neno na ndugu yako,iache sadaka yako hapo hapo UKAPATANE naye kwanza kisha urudi kutoa sadaka yako.
usilale na hasira kinyongo jua lisizame ukiwa na kinyongo hasira.
Ebr 12:14
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao
KUPENDA MALI KUABUDU MALI/KUTUMIKIA MALI badala ya kumtumikia Mungu kwa mali zetu.
Mathayo 19:20-22
Huyo kijana akamwambia, “Hayo yote nimeyazingatia; nifanye nini zaidi?”
Yesu akamwambia, “Kama unapenda kuwa mkamilifu, nenda ukauze mali yako, uwape maskini fedha hiyo, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate.” Huyo kijana aliposikia hayo, akaenda zake akiwa mwenye huzuni, maana alikuwa na mali nyingi.
Wakati mwingine mapenzi yetu kwa mali yanazidi mapenzi yetu tunavyompenda MUNGU na hii inakuwa ni kikwazo kwetu,ndio maana baadhi ya matajiri wanaotumikia MALI wanashindwa kumtumikia na Mungu kwa sababu ni vigumu kuwatumikia ma BWANA wawili utumikie mali na kimtumikia Mungu,lazima utampenda mmoja zaidi ya mwingine kati ya MALI na MUNGU.
Ndio maana unaona kijama tajiri alipoambiwa achague kati ya kumtumikia Mungu na Mali ,alifeli.
Hata leo ni wangapi wanampenda Mungu kwa nguvu zao zote,akili zao zote ,moyo wao wote ,na katika Roho na kweli kumuabudu kiuhalisi.
Ambao wamemuweka Mungu above all ,Mungu kwanza.
Mathayo 6:33
Lakini utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.
Ukiweka HAZINA yako hapa duniani na kuipenda dunia ,ndio na moyo wako utakapokuwa mahali hazina yako ilipo na kumpenda Mungu hakutakuwa ndani yako ,UTAIPENDA DUNIA badala ya kuweka hazina yako mbinguni ili moyo wako nao utakuwepo mbinguni.
MALI ni kitu kimoja katika vitu vingi vya duniani anasa na tamaa mbaya za miilli yetu ,tamaa za dunia zinatufanya tunakuwa WATUMWA wa anasa,watumwa wa mali,n.k pesa ndio inakuwa kila kitu kwetu kama BWANA kwetu badala ya Mungu ndio awe BWANA na kila kitu kwetu,na sisi tuwe watumwa wa BWANA Mungu yunakuwa watumwa tunakuwa watumwa wa tamaa mbaya za dunia hii na fahari zake badala ya kuwa watumwa wa Mungu na kumpenda na kuutafuta kumpendeza Mungu.
YAKOBO 4:4
hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu”.
1 Yoh 2:15-17
Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
***kumpenda MUNGU ni
***kishika AMRI ZAKE(UPENDO,penda Mungu+penda watu wote)
****kushika NENO LAKE. moyoni mwako..kuliishi kwa vitendo kifanyika upya neno likubadilishe moyoni mwako mpaka nje mwilini matendo yako yabadilike kama LAZARO MTOZAUSHURU alivyobadilika
Zakayo akamwambia Bwana, “Sikiliza Bwana nitawapa maskini nusu ya pesa zangu. Ikiwa nilimdhulumu mtu yeyote, nitamrudishia mara nne zaidi.”
9 Yesu akasema, “Leo ni siku kwa ajili ya familia hii kuokolewa kutoka katika dhambi. Ndiyo, hata mtoza ushuru huyu ni mmoja wa wateule wa Mungu.[a] 10 Mwana wa Adamu alikuja kuwatafuta na kuwaokoa watu waliopotea.”
KAMA hatutaruhusu kulipokea neno la Mungu moyoni mwetu na kumruhusu huyu NENO =YESU aingie moyoni mwetu ,= na kubadilika KUACHA DHAMBI..tutakuwa tunawasindikiza watu kwenda mbinguni wale wanaolisikia NENO na kulishika NENO katika roho na kweli ,wakiabudu kwa UHALISI
Mt 21:31 Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.