Habari wana Jamii Forums
Mimi kuna issue ambayo sijaielewa, yani dalali anatakiwa alipwe kodi ya mwezi mmoja na mpangaji kwa kumtafutia nyumba. Binafsi naona kumlipa dalali ujira kwa kazi ya kukutafutia nyumba ni kawaida kibinadamu cause ametumia muda wake kuzunguka kutafuta nyumba hiyo.
Tatizo linakuja pale dalali anapodai kulipwa kiwango sawa na kodi ya mwezi mmoja yani kama unalipa 500,000/= kwa mwezi basi dalali atapokea kiasi hicho hicho, huu ni wizi wa wazi kabisa.
Ingefaa kuwe na viwango maalumu vya kuwalipa madalali kama kwa asilimia na tena izingatie hali ya kipato cha watu maana yake mtu kwenda kupanga nyumba sio kwamba ana uwezo mkubwa sana kifedha bali kila mtu anajibana ili aweze kusogeza siku.
Wenye nyumba nao wanatakiwa kubadilika na kwenda na mabadiliko ya teknolojia ili kusaidia watu wanaotafuta nyumba, watumie platform zilizopo kama facebook, instagram au hata mitandao maalumu ya mitandao kama zoomtanzania. Watu wengi wanapitia mitandao hiyo na wala hawahitaji madalali kufanikisha kazi hiyo.