Kumkopa pesa masikini ni kujizalilisha

Kumkopa pesa masikini ni kujizalilisha

Junior Rutashoborwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2019
Posts
228
Reaction score
210
Habari zenu humu ndani,

Poleni sana na majukumu ya kila siku ya kuijenga nchi yenu mkiwa ndani...sisi huku nje tunaendelea kupambana ili kihakikisha tunaipeperusha vyema bendera ya Tanzania huku ughaibuni

Leo napenda ku-share nanyi kuhusu suala ambalo limenihuzunisha sana ndani ya wiki hii...kuna tetesi nimezisikia baadhi ya wafanyabiashara niliowaazima vijisenti wananitangaza huko nyumbani kuwa nimefirisika. Anyway, sitaki walaumu sana maana kila mtu ana mdomo wa kuongea.

Kama unapenda kutunza heshima yako usipende kuazima pesa kwa watu masikini ambao wamepata mali hivi karibuni (Self-made riches). Hawa jamaa wanadharau sana.

Kuna mzee mmoja namuheshimu sana ila alichonifanyia nimemshusha kuanzia leo. Anadhani kumiliki kiwanda cha vinywaji na mikate ametoboa bado sana.

Kuniazima dollar 2.6 million ndo akaamua kunitangaza. Kama hauna hela ya kukopesha watu kwanini usiwaambie kuwa huna? Sasa eti kila akikopwa utasikia " Kuna hela nimemkopesha mtoto wa Professor Rutashoborwa" ya nini yote hayo mzee wangu?

Mbona wenzako hawako hivyo....au umesahau kuwa viwanda vyako vya pwani nilikufanyia mchongo mzee wangu akakukopesha hela ukajenga? Au unadhani kwa ile business plan yako ungepewa USD 70 M? Jirekebisheni ++
 
Back
Top Bottom