Kumepambazuka! Wananchi na Ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumepambazuka! Wananchi na Ufisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Petu Hapa, Mar 26, 2009.

 1. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani eeeh!

  Mwenzenu haya magazeti yananipa opofu sasa. Hivi kila siku kiongozi huyu kasema kukicha yule kajibu, inamaana ni viongozi tu wanaongea! Sauti za wananchi ziwapi? Ama wao hawana maoni na mitizamo yao. Ni hatari sana kwenye mapambano kuacha viongozi tu ndio wanaonekanae wanayakusema, kama tunataka yawe mapambano ya kweli sura ya wananchi lazima itoke.

  RAI:

  Vyombo vya habari sasa vianze kuandika kwa kina wananchi tunasema nini kwenye ufisadi. Magezeti kichwa cha habari kikisema "vijana wa manzese waushikia bango ufisadi" sio viongozi tu watakaonza kutafuta pa kukaa, bali wananchi wengine watahamasika kusema kero na misimamo yao. Ni wakati wa kuonyesha vuguvugu limechemka hata kwa wananchi! Je wananchi wanaokerwa na ufisadi, wamechukua hatua gani! Wanajipanga vipi? Kunadalili zozote za wananchi kushinikiza au kuonyesha hawapendezwi na yanayoendelea!

  Kama unajua vuguvugu lotote la wananchi tafadhali weka hapa! Tuanze kupima joto, pia itatoa nguvu kwa wananchi wengine!
   
Loading...