Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,913
- 30,255
Kitabu hicho hapo juu ni moja ya vitabu katika mradi wa Oxford University Press (OUP) wa kufundisha wanafunzi wa shule za msingi lugha ya Kiingereza lakini pia wakati huo huo kuwafundisha wanafunzi hao historia za nchi zao.
Mradi huu ulichapa vitabu takriban 15 kutoka Afrika ya Mashariki lakini hapakuwa na kitabu chochote kutoka Tanzania. Ndipo OUP waliponiomba niandike kitabu katika mradi huu kwa ajiii ya Tanzania.
Kitabu hiki kilichapwa mwaka wa 2007 na hadi sasa kimeshachapwa mara mbili.
Bahati mbaya sana kitabu hiki hakikutiwa katika mtaala wa Tanzania ingawa OUP wamewafahamisha Wizara ya Elimu kuwa ni kitabu kizuri kitakachowasaidia wanafunzi kusoma Kiingereza na kujua historia ya uhuru wa Tanganyika.
Baada ya kushindwa kuingizwa kitabu hiki katika mtaala OUP walisimamisha kuchapa mswada wangu wa kitabu kuhusu Zanzibar, ''The School Trip to Zanzibar.''
OXFORD UNIVERSITY PRESS WATOA TOLEO LA PILI LA "THE TORCH ON KILIMANJARO" KITABU CHA WATOTO CHA MWANDISHI MOHAMED SAID