Kumbukumbu ya Eng Dr Abdullah Saleh Al-Harthy | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbukumbu ya Eng Dr Abdullah Saleh Al-Harthy

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Barubaru, Apr 17, 2012.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa wana ukumbi

  Kwa wote ninapenda kuwaarifu siku ya Al'Khamis 19 April 2012 kutakuwa na kisomo cha Hitma ya Mzee Sheikh, Eng, Dr Abdullah Saleh Al Harthy itakayosomwa katika sehemu mbalimbali .

  Hitima hizo sitasomwa baada swala magh'rib
  msikiti mkuu wa Mwera - Znz baada swala ya magh'rib
  Msikiti wa maamur Upanga.
  msikiti mkuu wa Urambo. Tabora Tz,

  Vile vile Msikiti wa Shaikh Idrisa, Lamu Kenya.

  Msikiti mkuu wa Al Azhar - Ontario Canada.
  msikiti mkuu wa Sallalah, Minal Fahal , Muscat Oman,
  Nyumbani kwa Balozi wa Oman DC na Ottawa Canada.
  Na kwengineko.

  Tunaomba tumuombee kipenzi chetu na mzazi wetu.

  Nitaweka historia yake hapo chini.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Buriani Alhaj, Engineer, Dr Sheikh Abdullah Salem Hamza Al Harthy
  Taarih 4 March saa kumi na mbili na dakika 20 alfajir saa za Oman, ndio ilikuwa siku ya mwisho wa uhai wa mzee wetu Dr, Eng, Alhaj Sheikh Abdullah Saleh Al Harthy. Msiba huu ulitokea nyambani kwake Salallah, Oman mara baada ya kumaliza kuswali swala yake ya Alfajir . Na kuzikwa siku hiyo taarih 4 March 2012 baada swala ya adhuhur.
  Ni msiba mkubwa sana usioweza kuzungumzika wa Baba yetu, ndugu yetu, mlezi wetu na kubwa zaidi ni mshauri wetu Mzee Eng Alhaj Abdullah Saleh Al Harthy.

  Mzee Abdullah alizaliwa mwaka 1934 huko Kianga, Mwera , Zanzibar , na kukulia Shangani Zanzibar kabla kuhamia kariakoo,Dar es salaam 1948. Alisomea skuli ya Sunni manzil vikokotoni Zanzibar kabla kuhamia skuli ya Habib Punja Muslim, Ilala Dar na baadae kuendelea na masomo katika skuli ya Kichwele na baadae Mzumbe Morogoro na Tabora skuli kabla kujiunga na burmigham University, UK na kumaliza shahada yake ya kwanza ya uhandisi wa mitambo na Umeme mwaka 1961.

  Miongoni mwa aliosoma nao ni Mh Iddi Mohammed Simba, Dossa Aziz, Marhum Alli Nabwa (aliyekuwa mwandishi maarufu sana wa habari Tz, na aliowahi kufanya nao kazi za kiandisi ni pamoja na Mzee Kazibure (Eng na alikuwa mwl Kibaha Sec), Prof Eng Awadhi Said Mawenya . na wengine wengi.

  Sheikh Abdullah ni miongoni mwa watoto sabaa wa Al Marhum Saleh Hamza Al Harthy, akiwa ni mtoto wa pili akifuatiwa na Hadji, Hudaifa, Zakiyah (ambaye ni mama yangu mzazi), Mohammed, Seif na Farhat akiwa ndio kifungua mimba wao.
  Sheikh Abdullah kama ilivyo kwa watu wangine rijaal alipata jiko mwaka 1957 akimuoa Bi Zayna Bint Alli Al Yahyai na baadae mwaka 1963 alioa mke wa Pili Bi Faharataj Bint Suleiman Al Mahshoum. Na kujaaliwa kupata watoto kumi na saba (17) ikiwa mke mkubwa watoto 9 na mke mdogo watoto 8.

  Katika maisha yake akiwa ndie First Engineer Tanganyika baada ya uhuru wake 1961 katika fani ya Umeme na Mitambo . Amewahi kufanya kazi sehemu mbalimbali kama wizara ya mawasiliano Tanganyika kama mhandisi mkuu mitambo, East Africa Post& telecommunication kama mwalimu na mkuu wa kitengo cha mawasiano ya anga (Radio and Transmission) chuo cha mawasiliano Mbagathi- Kenya.

  Mwaka 1976 aliamua kuondoka Tanzania na kurejea Oman kwa sababu za kisiasa. (Hapa alitofautiana na JK Nyerere kutokana kukataa kuingiliwa na siasa katika mambo ya kitaalamu ya kihandisi).

  Baada kufika Oman aliajiriwa Oman Telecom (OmanTel) kama Chief Engineer operations & Maintanance), kabla ya kuamua kujiunga na Ontario University (Canada )1978 kwa ajili ya Masters degree na baadae kurudi OmanTel na kuteuliwa kuwa Director of Network Planning and Construction.Wadhifa ambao aliendelea nao mpaka mwaka 1993 alipoamua kustahafu.

  Mwaka 1994 alichukuliwa na Ericsson kama Consultant katika project zao zote za Middle za (Installations and Maintenance). Mpaka mwaka 2002.

  Vile vile katika Umri wake amewahi kufundisha kwa muda katika vyuo mbalimbali kama Qaboos University, King Abdulazizi University, Uppsala University, Bangalore University India, Tata Institute India, Etisalat Academy UAE, Ericsson Academy Dublin na Ericsson ,South Africa, NTT East Institute Japan n.k

  Amekuwa registered katika bodi mbalimbali za kihandisi Oman, Canada, UK, India, UAE, Saudia , South Africa na Tanzania

  Mpaka umauti wake ameacha mke mkubwa na watoto 14, wajukuu 68, vitukuu 16 na watoto wa vitukuu 4 kutokana na uzawa wake. Miongoni mwa watoto wake 4 ni Ph.D holders, 3 ni wahandisi, 2 ni pilots , Mmoja ni Brig Gen jeshi la Oman na mmoja ni naibu waziri Serikali ya Oman. Miongoni mwa watoto wake watatu ni wafanya biashara nchini Tanzania na ni waTanzania kiuraia.

  Sheikh Abdullah ni kipenzi cha wengi sana. Na amewahi kujitolea katika mambo mengi sana hususan mambo ya Elimu. Ameshiriki sana kujitolea kujenga skuli mbalimbali huko Tanzania na Mombasa Kenya. Amelipia na kusomesha watoto na vijana wengi sana. Na amebahatika kwenda Hijja katika umri wake mara 33 na hija yake ya mwisho ilikuwa mwaka 2011.

  Vile vile amekuwa mtu wa kupenda kuitumia Elimu aliyopewa kwa ajili ya manufaa ya wengi. Yeye pia alikuwa mshiriki mzuri sana katika Midahalo na makongamano mbalimbali ya kijamii kama Mwambao, Zanzinet, Youngafricans forum, n.k.
  Kuna mengi sana ya kumwelezea lakin kwa leo nimeamua kukomea hapo. Tunaamini kuwa kila kilichozaliwa basi lazima kionje mauti. Nasi hatuna la ziada zaidi ya kumuombea Mola amlaze pahala pema peponi na kuzidi kumlipa kwa amali zake alizotenda hapa Duniani wakti wa uhai wake ikiwemo zile swadakat Jaaliya.
  Inna Lillahi wainna Illaihi Rajihunna.


  Dr Hamza Yousuf Al Naamani.

  Muscat Oman

   
 3. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Mzee Abdullah alizaliwa mwaka 1934 huko Kianga, Mwera , Zanzibar , na kukulia Shangani Zanzibar kabla kuhamia kariakoo,Dar es salaam 1948. Alisomea skuli ya Sunni manzil vikokotoni Zanzibar kabla kuhamia skuli ya Habib Punja Muslim, Ilala Dar na baadae kuendelea na masomo katika skuli ya Kichwele na baadae Mzumbe Morogoro na Tabora skuli kabla kujiunga na burmigham University, UK na kumaliza shahada yake ya kwanza ya uhandisi wa mitambo na Umeme mwaka 1961.

  Mwaka 1976 aliamua kuondoka Tanzania na kurejea Oman kwa sababu za kisiasa. (Hapa alitofautiana na JK Nyerere kutokana kukataa kuingiliwa na siasa katika mambo ya kitaalamu ya kihandisi).

  ..............Kama alizaliwa na kukulia Tanzania, iweje mwaka 1976 aliamua '' KUREJEA'' Oman? Ina maana hawa wazenj weupe hapa sio kwao ni wapitaji tu?................
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nimetumia neno la kistaharabu tu lakin kwa neno halisi ALIKIMBIA Nchi kukwepa madhila ya kiongozi mkuu dhidi ya wasomi wenye misimamo na wanaofuata maadili ya taaluma zao.
   
 5. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Asante Barubaru................maana nilishtuka kidogo
   
Loading...