kumbukumbu na vitabu

Explainer

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
516
504
Ushauri tu ndugu zangu.
Kwanza tunashukuru kwa kuendelea kupumua na kupewa nafasi nyingine ya uhai katika mwaka huu mpya.
Mara nyingi huwa napata mtihani na pia bado nimeyakosa majibu ya mtihani huo, hivi kwanini katika jamii yetu watu wengi hawapendi kusoma vitabu? Ama tuseme tutawezaje kutunza kumbukumbu na kujua matukio ki ufasaa zaidi bila vitabu!!. Sasa imefikia wakati kila kitu kwetu tunakiona kipya masikioni mwetu kwasababu hatuna historia yake, wala kuwa na uwelewa sahihi kuhusu jambo husika. Inaaminika kwamba ubongo hupata nafasi nzuri kujenga picha harisi kabisa ya kile unachokisoma katika kitabu, iwe ni hadithi flani au historia yoyote ya zamani sana au ya kisasa, taswila wazi itakayo jijenga akilini mwa msomaji ndio ukweli halisi wa tukio lenyewe analolisoma,
....Ndio maana hata wajuzi wa masuala ya historia za kale huweza kusoma kumbukumbu za matukio husika yaliyotukia tangu zamani na kisha kuyajengea taswila halisi na kutengeneza katika mfumo wa video, na sisi tulio wavivu kusoma vitabu huwa tunapata angalau nafasi hiyo kidogo ya kutafuniwa na kutizama kwa macho na sio kuusoma ukweli na kuujengea taswila kichwani mwako.
WAKUU tuchangie ili tupate elimu sahihi na kuvirithisha vizazi vyetu kwa maendeleo na utunzaji wa historia na tamaduni zetu
 
Back
Top Bottom