Papaa Muu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 243
- 292
Tarehe na Mwezi kama Leo ya Mwaka 1984, Taifa lilipatwa na majonzi makubwa. Jioni saa 11 kulisambaa taarifa kuwa Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Moringe Sokoine amepata ajali na kufariki dunia katika eneo la Dakawa akitokea Dodoma.
_____________
Edward Moringe Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa Mara ya Kwanza tarehe 13 Februari 1977 akiwa na miaka 38 tu( Alizaliwa August 1,1938). Ndio kusema alikuwa Waziri Mkuu akiwa kijana kwelikweli.
Anasifika kwa uadilifu na Uongozi makini huku nidhamu ikiwa Ndio msimamo wake hadi alipokutwa na Umauti kwenye ajali ya Gari tarehe 12 April 1984 katika eneo la Dakawa, Morogoro akitokea Dodoma.
Hayati Sokoine kama Kiongozi Mkubwa kijana hakuwa mtu wa kujilimbikizia Mali, Majivuno au dharau. Tunapoadhimisha miaka 35 tangu kifo chake, ni vema kutafakari jinsi gani Vijana tunaweza kuendelea kujitoa kwa nchi hii na sio maslahi ya mtu mmoja mmoja!
Kuweka kumbukumbu Sawa:
Hayati Edward M. Sokoine alihudumu kama Waziri Mkuu kuanzia Februari 13,1977 hadi Novemba 7,1980 kisha Februari 24, 1983 hadi 12 April 1984 alipofariki dunia. Hivyo alifariki akiwa na miaka 45 tu.
Kifo cha Sokoine kilimuumiza sana Baba wa Taifa, Mwl Julius K. Nyerere. Katika picha hiyo hapo chini, Mwalimu Nyerere akilia kwa uchungu mbele ya mwili wa Hayati Edward Moringe Sokoine.
https://www.facebook.com/FrancisDaudiTz/
Francis Daudi
Kaka Mkubwa!
12 April 2018.