Kumbe wanasiasa ndivyo mlivyo?

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,598
Kuwaamini wanasiasa ni kupoteza muda.... Hivi kweli watu wanakaa vikao kwa ajili ya kujadili maendeleo ya taifa, wanalipana mahela mengi, wanakaa vikao vya kujadili katiba, wanalipana mahela mengi ...
Linakuja suala ya kulipa kodi, watu hao hao wanasimama macho makavu bila aibu wanaanza kujivua nguo hadharani eti wao wasilipe kodi, hadi mkuu wao (rais) anatajwa kwenye wasiolipa kodi? Wale wenye kipato kikubwa sana (walitajwa bungeni); hawalipi kodi .. mara hii wanaangaika kuwafata walojenga vijumba vya kupangisha ili wajikimu na maisha magumu .. wanawabana eti walipe kodi.

Hivi watu hawa ni wanadamu au ni nini?

Hakika ubinadamu kazi ... kazi kwelikweli ....

KUMBE WATUNGA SHERIA NDIO WAVUNJA SHERIA????
 
Yaan wakikaa majukwaani wanavyo jionyesha kuwa ni wazalendo ,na kusema lazima tulipe kodi ili tuendelee kumbe wao hawalipi kodi.......unafiki huu.....mpaka lini halafu vijana wao wanakuja hapa kuwatetea ,eti wasilipe kodi
 
wanachimba kaburi LA chama au kufanya uchaguzi 2020 uwe mgumu sana kama 2015!!wananchi walikuwa tayari kuchagua jiwe kuliko mtu Wa chama kileeee
 
Tukisema tuiondoe CCM madarakani wengi sana huwa mnapinga humu ndani.

Angalau sasa watu wameanza kuona tatizo la hili dudu.
 
Tukisema tuiondoe CCM madarakani wengi sana huwa mnapinga humu ndani.

Angalau sasa watu wameanza kuona tatizo la hili dudu.
Hatuwezi kuitoa ccm madarakani, alafu tukawaweka madarakani lowasa na Sumaye,

Then tukadhani tuko salama
 
Tukisema tuiondoe CCM madarakani wengi sana huwa mnapinga humu ndani.

Angalau sasa watu wameanza kuona tatizo la hili dudu.
Tatizo sio ccm pekee..tatizo wte CCM na upinzan wanaangalia matumbo yao kwanza..uliona macho yalivowatoka walivoambiwa na wao wapigwe personal income tax
 
Tukisema tuiondoe CCM madarakani wengi sana huwa mnapinga humu ndani.

Angalau sasa watu wameanza kuona tatizo la hili dudu.
Tatizo letu hatuna alternative kuitoa ccm tunaileta ccm mlango wanyuma. kama una akili timamu wewe angalia kampeni ya mwaka jana Lowasa alipokua ana hati hati ya kushinda makada wenzake ccm walikua tayari kuja kujiunga naye, na sababu rais ana viti kumi ujue hao kumi wangeishia kuwa wana ccm wenzake ndiyo maana mimi simahamasiki na siasa za Tanzania tegemeo letu kubwa ni vijana wpya wasio na damu ya ccm siyo kina Mbowe na Lowasa. Ndiyo maana watu kama kina Mnyika, Tundu Lissu hawapewi nafasi maana kumejaa makada ya ccm wakijificha katika magwanda ya upinzani. Hebu angalia nani aliyeingia upinzani bila ya kufukuzwa ama kunyimwa kile alichokitarajia CCM. Mrema aliingia sababu alinyimwa nafasi ya Makamu Waziri Mkuu, Lowasa kaja CDM sababu kanyimwa kugombea urais kupitia ccm, Sumaye kaja CDM sababu alijua Lowasa akiukwaa na yeye kaula na watakua vinara wa upinzani, Ngombale ndo usiseme huyu kalelewa na ccm mwishoni kaona ccm inamtosa kama wazee wenzake walivyotoswa (kawawa R.I.P) akaona akimbilie kwa Lowasa. Lowasa kakosa urais Gombale haonekani, same kwa Mwapachu, sasa hapa kuna mageuzi gani utapata?
 
Back
Top Bottom