torvic
JF-Expert Member
- Mar 9, 2016
- 3,806
- 9,303
Ilikuwa kipindi kidogo holiday flani hivi, tumeenda beach na rafiki yangu akiwa na girlfriend wake. Kwenye kutembea tembea tukapishana na watoto wawili wa kike wakali kweli, wakiwa kwenye mikato ya kibeach.
Bwana rafiki yangu kujifanya ana shingo kama feni inazunguka pande zote na macho hayana pazia, akakodoa mijicho hiyo mpaka akaanzisha noma girlfriend wake akamwambia umewaangalia sana, umewaonao wazuri sana, lete simu nikupige picha nao rafiki yangu bila kuelewa akapiga nao picha na tabasamu pana.
Baada ya hiyo picha balaa lililotokea hapo ndio na mimi kupata msukumo wa kuandika huu uzi. Aisee yule girlfriend wa rafiki alicharuka kama Raisi na makontena ya madini kuanzia pale mpaka kwenye gari ilikuwa varangati, kwanini mjamaa aliwaangalia wale wasichana kama vile na kwanini alikubali kupiga picha, mwisho wa mchezo mahusiano yakakatika
Sasa vijeba wenzangu ukiwa na girlfriend/mchuchu wako kuwaangalia wasichana wengine mwisho mara moja tu, tena kwa kuibia tujikaze kwakweli.