Kumbe Selelii ni mdini na mkabila

Makelele

Member
Sep 23, 2007
28
4
Mbunge wa Nzega aingia matatani

Fidelis Butahe

MBUNGE wa Jimbo la Nzega mkoani Tabora, Lucas Selelii amelaumiwa kwa kauli anazodaiwa kutamka kwamba kila mtu anayetaka ubunge akagombee kwao na kwamba, mgombea wa Jimbo la Nzega lazima awe mkristo ili kuepusha kuibua suala la Mahakama ya Kadhi.

Selelii alinadaiwa kusema kauli hizo alipozungumza na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye hafla fupi aliyoiandaa baada ya kuwaita ili kubadilishana mawazo hivi karibuni na pia kwenye hafla ya siku ya wanawake duniani iliyofanyika mjini Nzega.

Alipoulizwa jana kwa njia ya simu, mbunge huyo alikiri kusema kwamba watu wa makabila mengine wanaotaka ubunge Nzega wasichaguliwe, lakini alikana kuzungumzia suala la udini.

Habari zilizolifikia Mwananchi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM mkoani Tabora zilisema, mbali na ukabila pia mbunge huyo alikuwa akiwashawishi watu mbalimbali kutokubali kumpigia kura mgombea ambaye sio muumini wa dhehebu la kikristo.

Mtoa habari wetu, alisema Selelii alidai wabunge wote waliokuwa wa Jimbo la Nzega walikuwa ni wenyeji wa mkoa huo, hivyo aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha kuwa jimbo hilo halichukuliwi na mtu ambaye sio mwenyeji wa Tabora.

"Maneno hayo aliyazungumza wakati akiongea na viongozi mbalimbali wa CCM, ambapo pamoja na mambo mengine alitutaka tusikubali kumpitisha mtu ambaye sio mwenyeji wa mkoa wa Tabora ili miaka yote wabunge wa hapa Nzega wawe ni kabila la Wanyamwezi," walisema watoa habari hizo.

Walifafanua kuwa hivi karibuni katika sherehe za siku ya wanawake duniani ambazo kimkoa zilifanyika katika kanisa la AICC lililopo eneo la Kariakoo, Selelii alitoa fedha taslimu Sh 270,000 kuwasaidia wanawake hao.

Lakini anadaiwa kwamba katika hotuba yake kwa wanawake hao aliwataka pia kutomchagua mbunge Muislamu kwani ataliibua upya suala la Mahakama ya Kadhi kauli ambayo Selelii amekana kuitamka.

Akizungumza na Mwananchi, Selelii alisema yeye alitamka wazi kwamba hatakubali kuona Jimbo la Nzega likichukuliwa na mtu kutoka nje ya Mkoa wa Tabora, kwa sababu kila mtu anatakiwa akagombee sehemu ambayo ni mwenyeji.

"Suala la udini mimi sikulizungumza kabisa, huo ni uongo, mtu wa dini yeyote anaweza kugombea isipokuwa awe ni mwenyeji wa mkoa wa Tabora, kama sio mwenyeji wa Tabora labda ametokea Bukoba akagombee hukohuko Bukoba hapa Nzega watagombea Wanyamwezi tu kila mtu ana kwao bwana," alisema Selelii .

Source: Mwananchi News
 
Hawa jamaa waliokuwa kwenye tume iliyochunguza RICHMONDULI watafuatwa fuatwa sana na vyombo vya habari vya hawa mafisadi!! Sasa tungoje ya Stella Manyanya nadhani wanamfanyia utafiti!!
 
MBUNGE wa Jimbo la Nzega mkoani Tabora, Lucas Selelii amelaumiwa kwa kauli anazodaiwa kutamka kwamba kila mtu anayetaka ubunge akagombee kwao na kwamba, mgombea wa Jimbo la Nzega lazima awe mkristo ili kuepusha kuibua suala la Mahakama ya Kadhi.

Tuletee ushahidi wa maneno au nenda kwa boss wako ukafanye kazi zingine. Utasikia ooooh mimi nimeiona tu kwenye gazeti jibu langu ni kuwa tumia akili yako siyo kila kitu unachokiiona au alichoankika Fide wewe unakicopy
 
Selelii katika jimbo lake la uchaguzi mwaka 2005 alibanwa mbavu na kijana anaetwa Hussein Bashe ambae hivi karibuni alikuwa mmoja wa wagombea wa UVCCM nafasi ya umakamu uenyekiti.

Hoja yake ya udini itakuwa anampiga dongo Bashe, swala la ukabila pia huyu Bashe ana asili ya kisomali, ktk uchaguzi na siasa za wilaya ya Nzega toka 2007 bwana mdogo huyu ameonyesha kumzidi nguvu sasa Selelii anaweza kutumia silaha hiyo ili kujijengea uhalali na kuweza kumvunja huyu dogo nguvu.

Lakini Selelii hali yake ya kisiasa sio nzuri dogo amemshika kubaya.
 
Huyu Bashe nasikia anafadhiliwa na Rostam kwa hiyo sioni ajabu kama Lucas kashikwa pabaya!! Nguvu ya KAGODA hiyo!!
 
Tuletee ushahidi wa maneno au nenda kwa boss wako ukafanye kazi zingine. Utasikia ooooh mimi nimeiona tu kwenye gazeti jibu langu ni kuwa tumia akili yako siyo kila kitu unachokiiona au alichoankika Fide wewe unakicopy

Umewahi kukanusha uliyoyasikia hapa ukumbini mara ngapi? Mara ngapi yaliyoletwa hapa yalibidi kuletwa kwa audio ndiyo ukayakubali?

ACHA PUMBA KWANI MAGAZETI YA MABOSI WAKO WEWE NDIO MISAHAFU?
Kama unaweza basi mtetee shujaa wako na shutuma zinazomkabili na sio kuwafokea walioleta habari hapa ukumbini.
 
Mtarajiwa.
source ni gazeti la Mwananchi kama angekuwa hajasema akilishitaki gazeti.hajakataa kuwa alikuwa kanisani na amewapa pesa kina mama wa kanisa ambao ndio wapiga kura na kampeni kwenye siasa ni kina mama.
 
Huyu Bashe nasikia anafadhiliwa na Rostam kwa hiyo sioni ajabu kama Lucas kashikwa pabaya!! Nguvu ya KAGODA hiyo!!

Nasikia wasiwasi wake unatokana na ukweli kuwa katika uchaguzi wa 2005 Selelii alifadhiliwa sana na RA lakini baada ya kupata akamgeuka. Sasa jamaa RA anataka ku revenge na kwa kuwa Lucas anafahamu fujo zake, basi ndio anaanza kujihami.

Asiwe na wasiwasi kwani kwa mfumo wa sasa waamuzi ni wananchi na sio matajiri wachache. Udini na ukabila hautasaidia... amwage sera tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom