Kumbe Polisi na Serikali waongo? Walisema Mwakyembe hakupewa sumu, leo Magufuli anasema alipewa sumu ili wamuue cha ajabu hawajakamatwa

Hakika ww una maelezo sahihi kuhusu hao jamaa na rais aliyepita. Je hili la Lissu, bensaa8 nk unalizungumziaje na huyu anayehusishwa?

Msimamo wangu ni kama Lissu siku alipohojiwa na BBC, Alisema Hana ushahidi wowote wa kuhusisha Serikal na Tukio lile
 
Kuna muda watatajana kuhusu Lissu hata kizazi chetu kikiwa hakipo wapo watakaoongea ukweli na uchunguzi wa kina utafanyika CIA na wengineo wataitwa watachora hizo gari na kujua jinsi walinzi wa lile eneo walivyoruhusiwa kuondoka siku ya tukio...Time will tell.
 
Msimamo wangu ni kama Lissu siku alipohojiwa na BBC, Alisema Hana ushahidi wowote wa kuhusisha Serikal na Tukio lile

Mbona amehojiwa sana na vyombo mbalimbali na mara zote amekuwa akimtaja mtu huyo huyo? Au hujasikia hayo mahojiano mengine bali hayo ya BBC tu kwani ndio yamekuacha wangalau na ahueni ukilinganisha na hayo mahojiano mengine?
 
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa jijini Mbeya wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi jijini humo iliyolenga kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Rais Magufuli amesema kuwa, "nimeambiwa Kyela kuna tatizo la umeme, kwamba umeme unakatikatika halafu kukatika kunaumiza sana, unakuta unaangalia mpira unakatika halafu goli ndiyo lilikuwa linaingia, na Waziri wa Michezo anatoka huku ingawaje kwenye timu ya vijana ameniangusha, yaani mpira uchezwe kwenye uwanja wako timu yako halafu mnatandikwa hapohapo yaani ajabu kweli".

"Vitu ambavyo vinaniboa ni kufungwa kwa timu zangu, huwa najisikia hovyo, natamani siku moja niwe Waziri wa Michezo halafu waone mimi nitakavyokuwa, timu nitaipanga mwenyewe" ameongeza Rais Magufuli.

Aidha kuhusiana na Waziri wa Habari, Utamaduni sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe Rais Magufuli amesema kuwa huenda watu wengi wa Kyela wakawa hawamfahamu kiongozi huyo.

"Mwakyembe alikuwa Naibu Waziri wangu alinisumbua sana, amewahi kunyweshwa sumu akapelekwa nje kwa sababu ya kusimamia haki, inawezekana nyinyi hamumjui Mwakyembe." amesema Rais Magufuli
Hivi Magufuli anadhani kupanga timu ya mpira ni kama uchaguzi wa marudio na vyama vya upinzani Tz? kwamba akiwa waziri wa michezo timu zetu zitashinda tu, kwa kuhonga refarii? au kwa kutumia Polisi? eeeh, polisi wanawakamata timu pinzani na timu yetu inafunga magoli!!!
 
Hili la Mwakyembe nakumbuka lilikanushwa sana na vyombo vya dola na serikali kwa ujumla kuhusu kupewa sumu, tena watetezi wakasema tuviamini vyombo vyetu vya uchunguzi. Leo rais wa nchi anasema ilikuwa ni sumu? Je hawa tunaowataja kuhusu shambulio la Lissu tuendelee kuviamini hivyo vyombo vya dola? Je wanaotajwa na Lissu ni uongo?
Anavyoongea utafikiri it was OK au jambo la kawaida tu.

Na ya Lissu tutayajua hivi hivi baada ya miaka kumi.
 
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa jijini Mbeya wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi jijini humo iliyolenga kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Rais Magufuli amesema kuwa, "nimeambiwa Kyela kuna tatizo la umeme, kwamba umeme unakatikatika halafu kukatika kunaumiza sana, unakuta unaangalia mpira unakatika halafu goli ndiyo lilikuwa linaingia, na Waziri wa Michezo anatoka huku ingawaje kwenye timu ya vijana ameniangusha, yaani mpira uchezwe kwenye uwanja wako timu yako halafu mnatandikwa hapohapo yaani ajabu kweli".

"Vitu ambavyo vinaniboa ni kufungwa kwa timu zangu, huwa najisikia hovyo, natamani siku moja niwe Waziri wa Michezo halafu waone mimi nitakavyokuwa, timu nitaipanga mwenyewe" ameongeza Rais Magufuli.

Aidha kuhusiana na Waziri wa Habari, Utamaduni sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe Rais Magufuli amesema kuwa huenda watu wengi wa Kyela wakawa hawamfahamu kiongozi huyo.

"Mwakyembe alikuwa Naibu Waziri wangu alinisumbua sana, amewahi kunyweshwa sumu akapelekwa nje kwa sababu ya kusimamia haki, inawezekana nyinyi hamumjui Mwakyembe." amesema Rais Magufuli
Msema kweli mpenzi wa Mungu. Na ukweli unatabia ya kumweka mtu huru.
 
Achana na huyu mropokaji , siku akishika nyaraka za TISS hakawii kumwaga mchele kwenye kuku wengi maana mdomo hauna speed governer.
Acha kumuita Rais wetu mropokaji... waheshimu watanzania...heshima kitu cha bure
 
Aidha kuhusiana na Waziri wa Habari, Utamaduni sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe Rais Magufuli amesema kuwa huenda watu wengi wa Kyela wakawa hawamfahamu kiongozi huyo.

"Mwakyembe alikuwa Naibu Waziri wangu alinisumbua sana, amewahi kunyweshwa sumu akapelekwa nje kwa sababu ya kusimamia haki, inawezekana nyinyi hamumjui Mwakyembe." amesema Rais Magufuli
Ajabu yaani watu wachague mtu ambaye hawamfahamu!!!! Au naye ni mmoja wa wabunge wa kutangazwa.
 
Umejuaje kama tukio analozungumzia Rais Magufuli ndio hilo hilo alilolizungumzia DCI Manumba?!

Hilo unalodhani ni tofauti na la DCI Manumba halikuishia kwa Dr. Mwakyembe kupelekwa hospital nje?? Kujifanya kujua kwingi ni shida kubwa kwako. Ungepaswa kuonesha haya ni matukio mawili tofauti. Sio kuomba mleta mada aeleze hilo. Swali lako halina maana!
 
Back
Top Bottom