Kumbe nilikuwa nakosea kumchukia Mkwere

Kumbe nilikuwa nakosea kumchukia Mkwere

Hbr wanajamvi
Nakumbuka enzi za uongozi wa Mh JK binafsi nilikuwa nachukia sana utawala wake kutokana na tuhuma za rushwa ufisadi.Cha kushangaza zaidi ezi za JK pamoja na hizo tuhuma maisha yalikuwa mepesi sana Mfuko wa saruji hapa mkoani kwetu ulikuwa Tsh 12500 leo 15000 Bati 12000-14000 leo 19500-20 na kitu,Sukari,Mafuta nk vilikuwa bei ya kwaida Watumishi wa Umma mishahara ilikuwa inaongezwa mshahara,WASTAAFU walilipwa kwa wakati maisha yalikuwa mazuri ya kumpendeza mungu.Leo hatuna wafanyakazi hewa,Mafisadi wamekomeshwa,hakuna ukwepaji wa kodi lakini cha kushangaza maisha ndiyo kwanzaa yanazidi kuwa magumu tatizo ni nini jamani
Maisha bora kwa kila mtanzania
 
Hata mm mpaka leo huwa sielewi kinachoendelea, naonaga kama mapicha picha tu
 
M
Nilidhani ukiondoa wafanyakazi hewa,ukaondoa ufisadi,kutowaongezea mishahara watumishi,kupunguza matumzi yasiyo ya lazima serikali itakuwa umeipunguzia mzigo serikali hivyo utapunguza hata kodi kwenye mambo ya msingi kama vifaa vya ujenzi nk
Mzee ruksa alisema hivi, kila nyakati na zama zake, vumilia tu yatapita haya cha msingi chapa kazi Kama nyuki.
 
Back
Top Bottom