Si ni shirika la umma na CCM ndio chama tawala. Ndio maana inatekeleza ilani ya chama tawala. Hata kama chama kingine kingekua madarakani wao wangetekeleza ilani ya hicho chama. Ndio maana akasema hivyo.
Kimaadili ya kitaaluma (professional ethics) viongozi wa idara za serikali na mashirika ya umma wao ni watendaji (technocrats). Hata kama wanatekeleza ahadi/ilani/sera za chama kilicho madarakani hawapaswi kutoa matamshi ya kisiasa. Wao wanapaswa kutumia taaluma zao kufanya yale ambayo wanaamini yataleta matokeo yanayotarajiwa kitaaluma. Ni matokeo hayo ambayo wanasiasa wanayatumia kujigamba kisiasa. Kwa hiyo huyo mtu wa NHC hakupaswa kutoa matamshi ya kukiunga mkono CCM. Lakini waTZ wengi hasa wenye umri uliosonga wana mgando wa mawazo au ufinyu wa uelewa wa demokrasia ya kweli. Kwa mtazamo wao CCM ikitoka madarakani hakutakuwa na serikali.Shirika lolote la umma duniani linatelekeza ilani za chama tawala