Kumbe Marekani inajisemesha mwenyewe. Haizungumzi na Iran

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,488
Reaction score
16,646
Vyombo vya ulinzi vya Iran na viongozi wao baada ya kuulizana wote wamesema hakuna mwenye taarifa ya kuwepo kwa mazungumzo na Marekani kama alivyosema raisi Trump ili kumalizia vita kati yao.

Kama madai hayo ni kweli basi Marekani tayari imepata ule ugonjwa tunaouona barabarani kwa watu wanaokuwa na upungufu wa akili pamoja na wale walliochanganyikiwa baada ya kupatwa na mkasa fulani,
Tamko la ugonjwa huo uliolipata taifa la Marekani limelotelewa na msemaji mkuu wa vikosi vya Khattam al anbiyai aitwaye Ebrahim Zolfaqari.
 
Huenda Pezeshkian anawazunguka wenzake anampigia simu Trump halafu akiulizwa na wenzake anajidai hajui nayeye😀
 
Huenda Pezeshkian anawazunguka wenzake anampigia simu Trump halafu akiulizwa na wenzake anajidai hajui nayeye😀
Ndio kwanza Marekani imepeleka madai yao.Kabla ya hapo hapakuwa na yeyote aliyekuwa na taarifa.
Haya mapendekezo hayana jipya.Ni yale yale na hakuna muirani atakayeyakubali.
 
Ndio kwanza Marekani imepeleka madai yao.Kabla ya hapo hapakuwa na yeyote aliyekuwa na taarifa.
Haya mapendekezo hayana jipya.Ni yale yale na hakuna muirani atakayeyakubali.
We ni Mu Irani?
 
Kwa nini tusiamini kwamba Iran wanafanya mazungumzo ya siri lakini hawataki ijulikane isije ikaonekana kwa waungwaji mkono wao kwamba wanasalimu amri kwa sababu haya mataifa ya kiislam yana katabia fulani ka kupenda yaonekane kwamba yako ngangari dhidi ya Marekani.

Naamini hicho ndicho kinachofanyika katika mazingara haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…