Ouuuuuukaaaaaaaayyyyyy ni hivi.
Wakati kijana mimi mdogo ndani ya Dar nikiwa naishi maeneo ya sehemu zilizochangamka toka enzi hizo nlitambulishwa kwa binti mmoja hivi mrembo aliyeletwa Home na dingi mdogo. Ni miaka ya kama 96 to 97 nafikiri ndo nlikuwa naingia kidato cha kwanza au form 2. Uhusiano wa mrembo huyu na uncle wala haukudumu kwa muda mrefu to a degree because bamdogo alikuwa kicheche.
Maisha yaliendelea na miaka kama mi 2 hivi ilikatika nikajakutana na yule mrembo. Ingawa yeye hakunikumbuka ila nilijitambulisha vyema akavuta kumbukumbu. Alinikaribisha Kinywaji kwenye bar moja iliyopo Jirani, kijana nkaichangamkia soda ya bure huku nikiwa na Uniform. Tulivyofika kwenye Bar hiyo alionekana mweji kupitiliza. Hata hiyo soda yenyewe aliingia ndani kwenye Fridge yeye mwenyewe na kuichukua.
Akantambulisha kama mdogo wake kwa wengine na kunijulisha kuwa yeye ni Barmaid pale. Mi nlishangaa kwani nilijua ni binti mwenye maadili yake na yeye nadhani aliona nashangaa kitu kama hicho akanikumbusha kuwa yeye na Bamdogo walikutana pale. Toka siku hiyo alikuwa rafiki yangu lakini sifa yake kubwa ya kubadili wanaume ilikuwa ikivuma mtaani. Baada ya miaka kama miaka 4 kupita nkakutana naye kwenye daladala alafu tukashuka pamoja nkawa natembea naye mimi nkielekea home lakini yeye akielekea kazini (Bar). Tulivyoachana baada ya yeye kufika jamaa mmoja akanifuata na kunistua dogo kuwa makini lile changu limeyakanyaga. Yasemekana kesha olewa na kuachika mara 2 na mume wake wa kwanza alikufa kwa ngoma. Hilo halipingiki kwani kila nilivyokutana naye tokea wakati ule alikuwa na mwanaume ambaye sikuwahi kumuona kabla. Alafu karibia wote walionyesha kuwa watu wazima. Baada ya hapo tukapoteana kwa kuwa niliondoka maeneo ya home nkaenda chuo na baadaye nkaanza maisha.
Jumaamosi hii maeneo ya Sinza nikiwa na washkaji wa kazini mchana kweupe mkubwa nikaagiza kinywaji, nashangaa kumuona Demu yule yule amekuja kutuhudumia. Yaani kazidi kunenepa na kaota makalio mazuriiiiiii alafu ngozi yake imekuwa nyeupeee kiufupi amezidi kung'aa. Miaka karibia kumi sijamuona lakini wote tulikumbukana. Akadai yupo pale kwenye ile bar mwaka wa 3 sasa.
Si kwamba namchulia ama namsema vibaya ila jamani nisaidieni japo kwa mawazo tu, Inawezekana kweli mtu auze K miaka karibia 20 alafu bado awe fit. Tukiangalia pakti za Condom zinasema Huzuia mimba na kupunguza maambukizi ya STD tena ikitumika kwa usahihi. Huenda akawa anatumia kinga if that is the case then Condom ni 100% safe kwa hili nimeamini. Amenipa mawazo mpaka naanza kufikiria kumbe Ukimwi haumuingii mtu kirahirahisi na hamna hata haja ya kuogopa sanaaa hili Gonjwa la hatari ilimradi mtu anatumia Condom utakuwa fit milele. Nilichojifunza ni kwamba mimi mpaka kufa kwangu aisee siji kutoka na barmaid. Nawaambia hata awe mzuri vipi simuangalii hata mara 2 (Haya mawazo yangu tu).