Kumbe hata wao wanaugua haya magonjwa

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
Shirika la afya duniani(WHO) linasema kwamba kuna ongezeko kubwa la kesi za ugonjwa wa surua zipo barani ulaya.

Zaidi yarobai na moja wameambukizwa katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2018.

Mwaka jana kulikuwa na kesi 23,927 na mwaka mmoja kabla kulikuwa na kesi 5,273.

Wataalam wa afya wanalaumu juu ya ongezeko kubwa la watu kuambukizwa ugonjwa huo ni kutokana na wengi kuacha kuzingatia chanjo.

Uingereza kumekuwa na kesi 807 mpaka sasa kwa mwaka huu.Shirika la afya duniani'WHO 'imeyataka mataifa ya ulaya kuchukua hatua thabiti

Wizara ya afya nchini Uingereza imesema mlipuko wa ugonjwa huo umetokana na idadi kubwa ya watu kusafiri katika maineo ya bara la ulaya ambayo yana maambukizi.

Surua inaambukizwa zaidi watu wakikohoa au kupiga chafya.

Maambukizi yanaweza kudumu kwa muda wa siku saba mpaka kumi.Lakini watu wengi waliopona kabisa huwa wanabaki na matatizo mbalimbali kama;

Madhara kwenye ubongo

Homa kali

Kupungua kwa mwili

Nomonia

matatizo la ini

Ni kwa jinsi gani ugonjwa wa ndui ulitokomezwa duniani?
Chanjo isiyo salama yaua Sudan Kusini
Utafiti uliofanywa miaka 20 iliyopita unaonyesha namna gani watu hawatilii maanani chanjo kama ilivyo kwenye matatizo ya utindio wa ubongo

Wizara ya afya nchini humo inawataka watoto wote kupata chanjo kabla hawajatimiza umri wa mwaka mmoja na kabla hawajaanza kwenda shule.

Ukraine ina idadi kubwa ya ugonjwa wa surua barani ulaya kwa watu zaidi ya watu 23,000 ambao wameathirika.

Lakini kuna nchi nyingine 6 barani ulaya ambazo zina maambukizi zaidi ya elfu moja.

Ufaransa

Georgia

Ugiriki

Italia

Urusi

Serbia

Na vifo vingi vilivyosababishwa na surua vimeripotiwa katika nchi zote hizo ,Serbia ikiwa inaongoza kwa idadi kubwa ya watu 14 kufariki.

Image copyright WHO
Image caption Ramani hii inaonyesha nchi 53 za barani ulaya ambazo zimekuwa na maambukizi ya surua tangu mwezi januari mpaka june.
________________________________________

Dalili za surua
Kuhisi baridi na kupiga chafya

Homa kali,uchovu,kukosa hamu ya kula na misuli kuuma

Macho kuwa na rangi nyekundu na majimaji kama unataka kulia

kuwa na rangi ya kijivu mdomoni

kuwa na vipele vyenye rangi nyekundu ambavyo vinaweza kusambaa kutoka kwenye kichwa,shingoni mpaka kwenye mwili wote.

________________________________________
 
Magonjwa hayo yalitusumbua miaka ya 1990's sasa hivi tupo kwenye mazungumzo na hili gonjwa la ukimwi soon tutaliondoa kabisa,wazungu wapambane na hali zao
 
Back
Top Bottom