Mududu
Member
- Mar 31, 2011
- 71
- 36
"Kwahiyo ndugu zangu, huu ni wakati wa kuyaua rasmi makundi. Uchaguzi umekwisha na sasa tuchape kazi. Na chama hakitamvumilia mtu yeyote atakaye endeleza makundi makundi". Ni baadhi ya ujumbe uliopatikana kwenye sehemu ya hotuba ya Ndugu M/kiti wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli.
Kauli inaonyesha makundi amabayo yalikuwepo ndani ya CCM kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, bado yapo na M/kiti ipo haja sasa ya kutumia taratibu, kanuni na sheria ili kumshughulikia yeyote atakaye yaendeleza. Nimefurahi kwamba hawa watu watashughulikiwa maana kama mnataka kwenda mbele, basi ni lazima WOTE muwe wamoja. Hata hivyo, katika maisha ya uhalisia, hili ni gumu sana kutokea.
Katika chama kinachijinadi kuwa na demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, kama alivyotanabaisha katibu wao mkuu, sikutegemea kuona hapatakiwi watu wenye fikra tofauti na kiongozi, au kupenda mtu mwingine tofauti na kiongozi. Tumexzoea kusikia tuhuma hii wakipewa vyama vingine, hususani CHADEMA, lakini kinyonga anachoweza ni kujibadirisha rangi tu lakini hawezi kuwa mjusi.
Hapa swali la msingi ni kwamba, kama bado kuna watu wanampinga mkuu ndani ya chama, inakuwa watanzania wengine wote nje ya chama wanamuunga mkono. Na akitokea anayempinga anavuliwa uzalendo? Au,,,kama kuna kupingana ndani ya chama, inakuwa tufike kwenye uchaguzi 2020 kukiwa hakuna upinzani. Kauli hizi zinatolewa kumzaamzaa tu sasa hivi ila zitaweza kuwa na maana baadae, kama alivyotabili Ndugu Makamba zamani juu ya ubatizo wa moto.