Kulinganisha gharama za tofali

Unazungumzia Dar ama mkoani?
Kama mkoani labda utanishawishi...

Ulitumia siku ngapi na hiyo mashine ukalipa 50,000 tu?
Je ni mashine ya mkono au vibrated?
Na je, kama ni mkono uimara wa tofali una uhakika nao kiasi gani?
Unaposema maji bure ulikuwa unachota mtoni? Na je mchotaji ni huyo huyo fundi au we mwnyewe?
Hakuna kisicho na gharama Boss.
Muda uliopoteza kusimamia unaweza kadiria Tsh ngapi?

Kwa Dar es salaam kufyatua tofali mwenyewe inaweza kuwa ni gharama kubwa kuliko haya ya kununua.

Binafsi nimefanya option zote hizi. Ila sitathubutu kufyatua mwenyewe tena. Maana ni presha na hasara sana nilipata.

Mapendo.
 
Mkuu ni wapi hapo unachajiwa sh 1000' garama ya tofali pamoja na kulisafirisha mpaka kwako. Na wanazingatia umbali wa kiasi gani?
Asilimia kubwa ya wauza matofali siku hizi wanatoa huduma za usafiri na kushusha kwa kuchangia kiasi kidogo sana, hardly Tsh 100 mpaka 200 tu kwa tofali...
 
Tofali moja ni 1050 × 2400 ni 2,560,000/= kufyatua mwenyewe utakuja kugharamika zaidi mbeleni...
Gharama ya tofali it is nothing kwenye ujenzi wa nyumba usiingie risk ya kupiga tofali mwenyewe km huna muda na uzoefu

Mhandisi
 
Acha roho mbaya mkuu.
Ha ha..usawa unabana, tunapeana ushauri angalau vibanda vyetu visogee, mimi niliitafuta jamaa wanitengenezee, jamaa wakawa wanatoa tofali 45 badala ya 30 niliyowaambia,mifuko mingine wanapiga, then jamaa mwingine nikampa kazi ya kumwagilia kila siku mara 2..akawaanamwagilia mara 1 na mimi ananiambia mara 2 ile pesa ya maji anakula yeye.
Matokeo yake hasara juu ya hasara...
 
Mkuu ni wapi hapo unachajiwa sh 1000' garama ya tofali pamoja na kulisafirisha mpaka kwako. Na wanazingatia umbali wa kiasi gani?
Maeneo yote ya Kigamboni,Kibada,Tuangoma...wauza matofali wengi sana wala huitaji kwenda mbali sana.
 
Daima
 
Huku kijijiji kwangu

Inchi 6 mpaka site 1100

Inchi 5 mpaka site 1000

Fanya mahesabu mwehyewe
 
Tofali moja ni 1050 × 2400 ni 2,560,000/= kufyatua mwenyewe utakuja kugharamika zaidi mbeleni...
Gharama ya tofali it is nothing kwenye ujenzi wa nyumba usiingie risk ya kupiga tofali mwenyewe km huna muda na uzoefu

Mhandisi
Kuna kitu watu wanshindwa kuelewa gharama za material hazibadiliki isitoshe unapata kazi ya kulinda tofali tena na muda unaongezeka unaweza kuta hapo ulipo hauna miundo mbinu rafiki kufyatulia tofali bora kununua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paragraph ya mwisho, umemaliza kila kitu na ndio ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo option ya kufyatua mwenyewe ni bad idea, imewahi kunipa hasara sana. Sirudii tena na siwezi kumshauri mtu
 
Tofali la sh 1000 hilo sio Tofali bali ni Tofali la biscuit! Nyumba imara nakushauri nunua Tofali la sh 1200-1400
 
Mimi kuna mtu eti alinishauri wakati wa kupaua nikanunue miti halafu nipasue mbao eti garama itapungua, mpaka leo sitaki kumuona machoni mwangu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…