Nakupa gharama zangu, nimefyatua tofali 2400.
Kukodi mashine 50000/=
Fundi kila tofali kufyatua ni tsh. 150/=(tulivyoelewana) jumla ni 360,000/=
Mifuko ya cement ilikuwa 71 jumla yake 923000/=
Usafiri mifuko ya cement sh.50,000/=
Mchanga Lorry 8 kubwa jumla sh, 420,000/=
Gharama ya maji ilikuwa bure.
gharama zote ni kama sh.1,803,000/=
Kama ningeamua kununua moja moja, tofali 2400.
Kila tofali linauzwa sh.1000, hivyo jumla ingekuwa 2,400,000/=
Kubeba na kushusha kila tofali ni sh.200/= ingekuwa jumla ni 480,000/=
Usafiri wa tofali zote trip kama 8 hivi kila trip sh.50,000/= ingekuwa 400,000/=
Jumla gharama zote kununua ingekuwa 3,280,000/=
Hivyo kwa ujenzi wangu niliokoa kama kiasi cha sh.1,477,000/=Hela ya fundi kunijengea boma
Conclusion: gharama hizi inategemea location, ulinzi nk. piga mwenyewe hesabu lakini kufyatua mwenyewe ni nafuu, kwa vile unaponunua, hata anayekuuzia gharama zake ameingiza humo kwenye bei yake.