Kulingana na ufafanuzi huu wa Rostam Aziz kuhusiana na umiliki wa Migodi unadhihirisha kuwa Polepole ametengeneza uzushi na kashfa chafu

Kulingana na ufafanuzi huu wa Rostam Aziz kuhusiana na umiliki wa Migodi unadhihirisha kuwa Polepole ametengeneza uzushi na kashfa chafu

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,992
Reaction score
5,660
Ufafanuzi wa Mh Rostam Aziz kuhusiana na umiliki wa Migodi unadhihirisha kuwa Polepole ametengeneza uzushi wa kuchafua biashara za Mh Rostam Aziz na inaweza kumgharimu Polepole kwa kiasi kikubwa huko mbeleni kwasababu anazungumza kwa kuzusha bila kuwa na ushahidi kamili

Baadhi ya Watanzania waliotizama mahojiano ya Rostam Aziz wamepata ufafanuzi wa kina

Shutuma kuhusiana na migodi, Mh Rostam anasema kuwa migodi mikubwa ya Tanzania inamilikiwa na kampuzi za Kimataifa kwa miaka mingi na wakati huo Mh Rostam alikuwa akifanya ukandarasi katika baadhi ya kampuni hizi kwa muda mrefu

Hayati Magufuli akamuuliza Mh Rosta kwanini na yeye asijaribu kumiliki biashara za migodi badala ya kuwa mkandarasi wa kampuni za nje kwa muda mrefu ndipo Mh Rostam akapata wazo la kujaribu kumiliki

Mh Rostan hakununua share za Serikali kama anavyozushiwa na watu wenye chuki dhidi yake badala yake alikwenda kununua share za kampuni hizo za nje ya nchi ikiwemo Australia na Marekani kwasababu ndiko liliko chimbuko la Kampuni hizo na alinunua kwakufuata taratibu zote za uwekezaji wa Kimataifa

Mh Rostam anasema kuwa aliuziwa share nje ya nchi kama wageni wengine wa Kimataifa wanavyouziana share za kampuni hizi wakiwa nje ya nchi, na tofauti kubwa na wawekezaji wengine wa nje ya nchi ilikuwa asili yake ya Tanzania

Mh Rostam anasema kilichofanyika ni Kampuni hizi za Kimataifa ambazo zimekuwa zikimiliki migodi hii kwa muda mrefu kuamua kuuza share zao kwa wamiliki wapya lakini kwasababu alikuwa na uwezo wa kununua akafanikiwa kupata umiliki

Mh Rostam anasema kuwa badhi ya migodi mfano mgodi wa makaa ya mawe bado hajaanza kuchakata makaa ya mawe kwasababu mpaka sasa anaendelea kukamilisha taratibu za umiliki hivyobasi uzushi wa kuwa makaa ya mawe yanauzwa na Mh Rostam unafaa kupuuzwa

Kuhusu matumizi ya makaa ya mawe kutumika kuyeyusha vyuma kama baadhi ya Watanzania wanavyodai sio ya kweli kwasababu makaa yanayovunwa sasa yanakwenda kutumika kuendeshea viwanda nje ya nchi kwa mujibu wa maelezo ya Mh Rostam

Mh Rostam anasema kuwa anapokea shutuma mbaya kutoka kwa Watanzania wenye roho mbaya ikiweno Polepole kwasababu wana chuki juu ya yeye kufanikiwa kuwa na uwezo wa kufanya biashara kubwa ambazo Watanzania wamekuwa wakiamini hawawezi bali wageni ndio wenye uwezo huo peke yao


View: https://youtu.be/twTNb51Vu0A?si=-VQYuVidvVf8VTce
 
Kama ndivyo, wamuache Ndugu Lisu huru, aje atuambie kama haya anayosema huyu dalali ni ya kweli.
 
Utetezi wake umekaa kijinga sana,anataka huruma kwa watanzania huku anatuibia,ni bahati mbaya tu hii nchi haina vyombo strong vya kuwachunguza hawa matajiri untouchable,wangebaini uozo mwingi sana.Kwa nchi zinazojitambua kuwa na kashfa tu ni shida kubwa either ni kweli au si kweli
 
Why is this about Polepole na Fulani na sio Shutuma za Wizi au Lah... Ndio huenda makaa ya mawe ni uzushi je kuhusu lobbying na watanzania kuchezewa na Nishati Safi kwa kuuziwa Nishati ya gharama (kwa manufaa ya wachache) na kukatazwa ya bure (Kuni) wakati kuna mbadala (Umeme)
 
Unamwamini Rostam?
Anadai kuwa migodi amenunua share kutoka kampuni za nje na sio share za Serikali kama wanavyomzushia lakini pia anasema bado hajaanza kuchakata makaa ya mawe kwasababu bado anakamilisha taratibu za umiliki, kwako hii imekaaje?
 
Rostam wanamuandama bure hana kosa.Anatumia skills na mtaji wake kuwekeza sio tu Tanzania mpaka nje ya mipaka ya Africa.
Mbona Mo na Bakhresa wamewekeza nje ya mipaka ya nchi na hawapigiwi kelele kama huyu dalali wa nchi Rostam!!?? Na kwa nini ang'ang'anie kufanya biashara na serikali!! Kuna walakini hapa tutake tusitake
 
Write your reply...watu wameamua kuchagua upande ndugu hata uwaambie ukweli vipi wao hawatakubali maana wameshajazwa chuki na chuki huleta upofu kila kitu hawatakiona chema kwa huyo wanao mchukia
 
Aliula mgodi wa dhahabu nzega resolute mining ilikuwa ikionekana kampuni mama, Caspian(taifa group kwa sasa ama ukipenda ita Rostam) ikionekana Contractor, kumbe ilikuwa kampuni Moja!

Kama ulifanya kazi resolute kama mimi kabla dhahabu haijaisha 2005 mwishoni, utanielewa!..ni kati ya migodi iliyodumu kwa kipindi kifupi sana.
 
Aliula mgodi wa dhahabu nzega resolute mining ilikuwa ikionekana kampuni mama, Caspian(taifa group kwa sasa ama ukipenda ita Rostam) ikionekana Contractor, kumbe ilikuwa kampuni Moja!

Kama ulifanya kazi resolute kama mimi kabla dhahabu haijaisha 2005 mwishoni, utanielewa!..ni kati ya migodi iliyodumu kwa kipindi kifupi sana.
Huyu ni mwizi wa dhahiri wala huhitaji elimu kubwa kujua,na wanaomtetea ni watu wasio na huruma na hii nchi,kwa bahati mbaya sana mifumo yote ya ulinzi na uchunguzi iko corrupt.Tutaziokoa vipi rasilimali zetu zitunufaishe watanzania!!? So sad
 
Anadai kuwa migodi amenunua share kutoka kampuni za nje na sio share za Serikali kama wanavyomzushia lakini pia anasema bado hajaanza kuchakata makaa ya mawe kwasababu bado anakamilisha taratibu za umiliki, kwako hii imekaaje?
Very likely he is lying. Amebobea kwenye deception na mambo mengine ya kijasusi.
 
Kuna ka ukweli ndani yake! Kama amekuwa akifanya biashara kubwa ambazo watanzania tunaamini hatuwezi tusimpuuze.
Hata Wazungu walifanikiwa kutu colonize na kuiba raslimali kwa kutufanya hawezi kuzichimba!
Ngoja tumngoje Polepole atajibuje.
 
Kuna ka ukweli ndani yake! Kama amekuwa akifanya biashara kubwa ambazo watanzania tunaamini hatuwezi tusimpuuze.
Hata Wazungu walifanikiwa kutu colonize na kuiba raslimali kwa kutufanya hawezi kuzichimba!
Ngoja tumngoje Polepole atajibuje.
Mgodi wa Makaa ya Mawe alioununua kwa Billion 5 ni Biashara ambayo Watanzania wengine wanaamini hawawezi kufanya?
 
Back
Top Bottom