Kulikoni TFF na uwnaja wa Taifa

Rabin

Senior Member
Mar 21, 2009
181
39
Poleni na majukumu wadau, naomba nizungumzie kitu ambacho nimekiona na kimenikera wakati wa mechi ya taifa stars na morocco.

Kwanza: Utaratibu wa ukataji tiketi, hivi kweli kwa hadhi ya uwanja tulionao sasa hivi ni busara kukatia tiketi kwenye daladala? Hivi uwanja hauna sehemu maalum ya kukatia tiketi au mawakala maalum kwa ajili ya kazi hiyo? Wale jamaa wanakaa ndani ya daladala hivi wamewekwa na nani maana hata mwendawazimu anaweza kufikiri tu kwamba kama kuna mtu alitoa wazo hilo la ktumia daladala basi kuna mchezo mchafu pale, hilo limenikera na ni aibu sana kwa watanzania.

Pili: Nilikata tiketi ya shilingi 10000 nilipofika mlangoni nikakuta mabaunsa na mapolisi wa ffu wakaniita wakaniambia kama nataka kukaa kiti cha 20000 basi niwape 5000, sasa hivi tunakwenda wapi, hawa wanajinufaisha na hizi 5000 huu uwanja ni baba zao? Na wana jeuri kweli!!

Tatu: Uchafu, hivi tff wanafanya nini uwanja tumejengewa mzuri hata kufanya usafi wa viti kabla ya mech hakuna? Kwenye corridor zote ni chupa za maji na soda na vumbi lisilo na kifani, na vip kuko hivyo? Hivi nchi hii usanii utaisha lini jamani? Ifike mahali tubadilike

naomba wadau tuyakemee haya
 
mmh! aibu na wameshazoea, ndio maana tunafungwa nyumbani, mazingira machafu, wimbo wa taifa unagoma hapo tu morali ya wachezaji inashuka kwa takribani % 40. mpaka ikirudi tumeshalala na mchezo kwisha
 
Back
Top Bottom