Kulea mtoto ni zaidi ya kumtimizia mahitaji na kumpenda, Wamama wa kisasa ni ngumu kulea watoto wa kiume, wapeleke watoto kwa wanaume kujengwa kitabia

Kulea mtoto ni zaidi ya kumtimizia mahitaji na kumpenda, Wamama wa kisasa ni ngumu kulea watoto wa kiume, wapeleke watoto kwa wanaume kujengwa kitabia

nguvu ya buku

Senior Member
Joined
Jul 15, 2025
Posts
168
Reaction score
549
Watu wengi huwa wanadhani kulea mtoto ni kumpenda na kumtimizia majukumu kama chakula, nguo, elimu na matibabu.

Kulea kunahusisha pia kitu muhimu kumjenga mtoto kitabia,

Kina mama wengi wa kisasa hawawezi kumjenga mtoto wa kiume kitabia kwasababu wao ni wanawake na mazingira yamekuwa yenye utandawazi mkubwa sana tofauti na zamani.

Mtoto wa kiume atapendwa sana na mama yake, atatimiziwa majukumu na baba yake au mama yake lakini anamuhitaji mwanaume kujengwa kitabia

Mtoto wa kike atapendwa sana na baba yake, atatimiziwa majukumu na baba yake au mama yake lakini anamuhitaji mwanamke kujengwa kitabia

Na ndio maana hata nchi zilizoendelea kuna wanawake matajiri wanapenda watoto wao, wanawatimizia majukumu lakini watoto wanajengwa kitabia kwa kujifunza mitandaoni, huko mitandaoni si salama kuna watu kama kina Andrew Tate wapo hard core sana.

Mama hayupo tayari kumuacha mtoto ili amkomoe baba yake au aendelee kupata hela za matunzo lakini anaemkomoa zaidi ni mtoto wake, mtoto anakua clueless bila mwanaume anaeweza kuwa kioo kwake.

Hata kama baba hayupo ni heri mtoto awe anaenda kwa ndugu wa mama watu wazima wanaojitambua kidogo kama wajomba, ikipendeza alipie matumizi akiwa huko.
 
Back
Top Bottom