Kukuacha sitajaribu

Kukuacha sitajaribu

Ushimen

Platinum Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
44,836
Reaction score
113,220
Naapa kutoadhibu, mpenzi hutoudhika,
Nitakwondoleya tabu, ukabaki wapendeka,
Nibaki wako tabibu, hino raha kukuvika,
Mrembo unapendeka, kukuacha sijaribu!

Wanambiya ya ajabu, ubongo nakanganyika,
Nishakupa langu jibu, kwa urembo wapendeka,
Miye sitoghilibu, ukweli utatendeka,
Mrembo unapendeka, kukuacha sijaribu!

Sijaipata aibu, kwa lote linatendeka,
Sikulipi kwa adhabu, kwangu unahitajika,
Ninaifanya sulubu, ukipate cha kulika,
Mrembo unapendeka, kukuacha sijaribu!

Katu sitakuwa bubu, nataka kueleweka,
Ninakupenda muhibu, wewe ni wangu rika,
Alinieleza babu, kitukuu anataka,
Mrembo unapendeka, kukuacha sijaribu!

Nahifadhi kwa vitabu, sifazo za kutukuka,
Nakupendea adabu, kwa mambo ninayotaka,
Kila swali lina jibu, jambo likihitajika,
Mrembo unapendeka, kukuacha sijaribu!
 

Best nimeitika wito, juu ujumbe mie ndo mlengwa au.... Maana sijaelewa bado nashangaa shangaa maana the intended girl must be lucky.... .
Lucky her...... Sio siri ushiboy anajua kupenda, kucare, kutunA, kubembeleza na........ Ila tuu ukimuudhi akaamua kukutosa basi ujue imekula kwako akikusamehe mtabaki kuwa marafiki la anakuchunia kimoja.

Samahani ushiboy kwa kutoka siri zako bila ruhusa yako. Missing u in those days.
Kasie.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom