Kukua kwa uchumi wa mtu ni zaidi ya kufanya kazi kwa bidii

Bob12

JF-Expert Member
Feb 27, 2017
11,422
58,787
Habari wana JF

Kila mtu anapenda kuona uchumi wake unakua siku baada ya siku na ndiyo mana watu wanafanya kazi usiku na mchana(walio jiajiri na walio ajiriwa) ili kujikwamua kiuchumi,lakini unakuta walio wengi wanapiga hatua kidoga sana tofauti na nguvu kubwa wanayowekeza ktk kufanya kazi.

Tatizo ni nini?

1) Matumizi ya pesa unayoipata iwe nyingi au kidogo ndiyo yatakufanya upige hatua kubwa,ndogo au ubaki pale pale kila siku na pengine kushuka zaidi.

Hakuna mtu anayefanikiwa kama hana heshima na pesa anayoipata haijalishi ni kwa kiasi gani anapata ila ni namna gani anaweza kuimudu,kama huna matumizi mazuri ya pesa utabaki pale pale au kupiga hatua kwa kiasi kidogo sana.

2) Tatizo lingine ni kutotambua wakati ulionao unatakiwa uutumie vipi,kuweka malengo ya muda mfupi na muda mrefu.
Mfano:-
Wewe ni kijana ambae unafanya kazi na hauna majukumu mengi sana,usipojenga muda huu,usipowekeza katika miradi lazima utapata sana shida pindi utakapokua na majukumu makubwa ya kifamilia. Maana itakubidi,ulishe familia,usomeshe watoto,ujenge,uanzishe miradi ya kiuchumi,ongeza na michango mbali mbali ktk jamii inayokuzunguka. Mwisho wa siku unapata presha.

3) Kujenga imani kua ipo siku utafanikiwa pasipo kua na mikakati maalum,kaa ukijua hakuna muujiza kama huo,hakuna.

Nini kifanyike ?

Lazima uweze kumudu matumizi ya fedha unayopata ikibidi uwe na mipangilio thabiti.Katika fedha unayoipata hakikisha

1) Unampa Mungu sehemu ya kumi ya fedha yako.
Soma Malaki 3:8-10
Usipotoa hiyo mana yake unamuibia Mungu na ukitoa amesema atakufungulia baraka tele.

2) Tenga fungu maalumu kwa ajili ya fedha za biashara,aidha kufungua au kuendeleza biashara.

3) Tenga Fungu maalum kwa ajili ya dharura km ugonjwa,michango nk.

4) Tenga fungu maalum kama akiba(A part of what u earn is yours to keep).

Ndugu zangu hayo ni machache tu kati ya mengi ambayo yanaweza kutufanya tukue kiuchumi,nadhani kila m1 ana wazo lake ambalo litatusaidia sote ktk maisha.

Asante
 
Hilo fungu la 10 tulilishwa ujinga na wakoloni kwa Maslahi yao. Sidhani kama Mungu wa kweli anahitaji fedha maana yeye hafanyi miamala ya kununua bidhaa au huduma
 
Hilo fungu la 10 tulilishwa ujinga na wakoloni kwa Maslahi yao. Sidhani kama Mungu wa kweli anahitaji fedha maana yeye hafanyi miamala ya kununua bidhaa au huduma
Inawezekana mkuu,ila toka nianze kutoa hilo fungu sijawahi kujuta
 
Back
Top Bottom