Kuku wa nazi

Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
26,303
50,470
Mahitaji:
1. Kuku aliyeandaliwa

2. Tui la nazi

3. Kitunguu thomu

4. Kitunguu maji

5. Pilipili mboga

6. Pilipili manga/mbuzi
karoti

Upishi:
Mchemshe kuku wako na uweke pilipili mbuzi, na kitunguu swaumu na chumvi kisha saga karoti, kitunguu maji, pilipili mboga pamoja, kuku akianza kuwiva tia mchanganyiko wako hapo juu kisha subiri kidogo utie tui la nazi acha ichemke dakika tano na tayari kwa kuliwa waweza kutumia majani ya giligilani kwa harufu murua.

TIPS: Usichemshe kuku na maji mengi sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom