BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,766
- 23,230
Kuku wa kuoka haleti kitambi kama wa kukaanga. Sasa hivi nimeingia msituni, ni kuoka mwanzo mwisho. Nimeambiwa kuna hadi maandazi ya kuoka, hebu nitonyemo kama unajua.
Asante sana mwalimu Gaijin
sasa yanapikwa kama scones? Na kuumua ni mara moja,manake scones huwa naumua mara mbili. Baada ya kukanda naacha unga uumuke kwanza to twice the volume, nakanda na kukata na kupanga na kuacha ziumuke mara ya pili ndo nioke.
Unaumua mara moja tu.
Ukishakukanda unga, kata, tandika sehemu yako vizuri, panga, yafunike mpaka yaumuke, choma jikoni.
*Hapa labda nikuulize, maandazi ya kuchoma kwa mafuta kawaida kwani unafanyaje?
Hayo huwa nayaumua mara moja na nachanganya yeast na baking powder. Nikishakanda nakata immediately, yakiumuka ndo nachoma.
Mkate ndo naumua kwanza, nakata uumuke mara ya pili ndo nikate.
Kuku wa kuoka haleti kitambi kama wa kukaanga. Sasa hivi nimeingia msituni, ni kuoka mwanzo mwisho. Nimeambiwa kuna hadi maandazi ya kuoka, hebu nitonyemo kama unajua.
Combinenga recipe hii hapa kwa mabachela: humo kwenye baking tray ya kuku unawekelezea viazi vitamu ama mbatata vilivyokatwa size mara mbili ya chipsi.
Dakika 10 kabla ya kuiva kuku na viazi, weka carrots, brocolli, koliflower, hoho na vitunguu vilivyokatwa vikubwa kiasi na endelea kuoka. Ukitoka hapo una full meal, kachumbari na juice mambo shega.
Na bata mzinga je?
Maandazi ya kuoka yapo ya aina nyingi ila mbili kati ya hayo ni
1. Ya kukatwa na kuchomwa kwenye tray (kama ulivyooka kuku)
2. Ya sufuria aka mahamri
Kwa yaliyokatwa, ponda unga wako maandazi kama unga wa maandazi ya kukaanga kwa mafuta (tafadhali tumia yeast badala ya baking powder, na fanya Unga uwe mwepesi zaidi ya maandazi ya kukaanga)
Kata katika size upendazo, funika kitambaa katika sehemu yenye joto, hadi yaumuke (unayaona yanakuwa mepesi, na ukiyabonyeza hayarudi)
Panga kwenye tray yako iliyopakwa mafuta, choma kwenye pre-heated oven (200C) hadi yatakapogeuka rangi ya kahawia.
Toa jikoni, yapake maandazi yako mafuta while hot (chovya brush yako kwenye mafuta kidogo kisha pakaa maandazi-itasaidia kuyafanya yasikakamae)
Yakipoa, tayari kwa kula
Note: unaweza kufanya ya chumvi pia badala yake ukipenda
Hayo huwa nayaumua mara moja na nachanganya yeast na baking powder. Nikishakanda nakata immediately, yakiumuka ndo nachoma.
Mkate ndo naumua kwanza, nakata uumuke mara ya pili ndo nikate.
nice one mkuu nimeipenda hiyo na kuhusu mafuta unatumia yalioganda yaani tanbond au ya kawaida kama alizeti?
bata na bata mzinga na jamii zao sijawahi kula wala kupika....labda king'asti atusaidie kama ana utaalam eneo hilo
Lol. Bata mie najua wa kuoka tu na anakuwa stuffed japo mie sipendi kula.
Unampaka bata mzima mafuta na viungo vyote kama chumvi, swaumu, binzari, tangawizi na ndimu. Unaweza kumlaza kwenue friji ama akae masaa kadhaa akikolea viungo.
Stuffing ni kumjaza tumboni, unaweza kuweka wali (njia bomba ya kula kiporo kwa furaha zote,lol) uliochanganywa na viazi, njegere, vitunguu na bread crumbs.
Oka kwa lisaa limoja ama endelea kuangalia abadilike rangi. Muhimu uchanje kuangalia kama bado ana damu manake.kama bata ana umri sawa na wewe ni kasheshe.
Hapo kwenye maandalizi ya bata umesahau kumtahadharisha kuhusu kufunga mdomo wkt wa kumnyonyoa. Maana akisahau hilo aweza kuta akatumia siku nzima kunyonyoa mpaka hamu ya kula iishe