Kuku vibudu wanaoliwa Dar

Kibiti1

Senior Member
Jan 19, 2017
126
127
Siku za hivi karibuni nimekutana na matukio mbalimbali ya kuku waliokufa aidha wakati wa kusafirishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingi au ajali mbalimbali. Nilidhani kuwa utaratibu ule wa zamani kuku akifa ni kibudu huwa haliwi lakini mambo sasa yanasemekana kuwa tofauti, katika kufuatilia nikakuta wananunuliwa tu kama kuku wazima japokuwa bei inapungua kidogo.

Mwisho katika kufuatilia nikaambiwa kuwa kama umeshawahi kula chipsi kuku kunauwezekano mkubwa ukawa umewala kuku hao. Mwili ulikuwa kama umekufa ganzi jamani!

Naomba mnisaidie, nawezaje kugundua nyama ya kuku kibudu kabla sijala?
 
kumbe makonda na ziro wanakula hawa duu
d923a9eaef51653894ac79928d21d738.jpg
 
Back
Top Bottom