Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Ngoja nitoe shule kdg kwa Wafuasi wa chama chakavu,
Duniani Popote ambako kuna mfumo wa utawala kuna makundi matatu ya watu. Utafiti uliofanywa na Proffesor Tiffany Brannon wa Chuo Kikuu cha Carlifonia unaonesha kuwa mahali popote penye mfumo wa utawala iwe ni utawala wa nchi, kijiji, taasisi etc watu wake wapo katika makundi matatu.
Professor Branon ambaye ni mbobezi wa Sayansi ya Tabia na Saikolojia (Behaviour Science &Psychology) ametaja makundi hayo kama ifuatavyo;
1. #Accorders;
Hawa ni wale wanaounga mkono karibu kila kitu kinachofanywa na utawala. Hili ni kundi la WASIFIAJI wa Utawala, Mfumo au Serikdali.
Utafiti wa Professor Brannon unaonesha wapo ambao husifia kwa KUPENDEZWA na utawala unavyofanya kazi na wengine husifia ili KUJIPENDEKEZA kwa utawala. Wanaosifia ili kujipendekeza kwa utawala ni wengi zaidi kuliko wanaofisia kwa kupendezwa na utawala.
Wale wanzosifia ili kujipendekeza hawapendi kureason. Kila wanachokiona kwenye utawala wao ni kusifia tu. Wale wanaosifia kwa kupendezwa na utawala huwa wanareason.
2. #Dissenters;
Hawa ni wakosoaji wa mfumo. Mara nyingi hutafuta madhaifu ya utawala ili kupata uhalali wa kukosoa. Wengi katika kundi hili ni watu wanao-reason sana japo wapo wachache wanaokosoa bila kureason. Watu wa kundi hili hutafuta kosa lolote katika utawala na kulifanya agenda.
Wanaokosoa kwa kureason hufanya hivyo kwa nia njema, lakini wanaokosoa bila kureason huweza kuwa na nia mbaya.
Wanaokosoa kwa nia njema hulenga kuikumbusha serikali wajibu wake katika kuboresha maisha ya wananchi. Tafiti zinaonesha kuwa tawala zilizokuwa na Wakososoaji wengi (Dissenters) zilifanya vizuri sana kuliko tawala zilizoendekeza wasifiaji (Accorders).
Katika nchi zilizoendelea "Dissenters" huwa ni wasomi, wanazuoni/wanataaluma au watafiti wabobezi. Lakini katika nchi maskini wasomi wengi huogopa kukosoa kwa hofu ya kuwajibishwa.
3. #Latents;
Kundi hili ni la watu ambao wapo "neutral" kuhusu mfumo wa utawala. Hawakosoi wala hawasifii. Wao husubiri hoja kati ya "Accorders" na "Disenters" na wakishawishiwa kwa hoja huunga mkono kundi mojawapo. Utafiti uliofanywa na Proffesor Brannon unaonesha kundi hili ndio lenye wafuasi wengi zaidi.
#MyTake.!
Kutokana na utafiti huo hapo juu bila shaka kila mtu anaweza kujithmini na kujua yuko kundi gani.
Kama upo kundi la kwanza, la pili au la tatu si kosa, ila kosa ni kuona waliopo makundi tofauti na wewe wamekosea. Kwa mfano ww ni msifiaji lakini hutaki kuona wakosoaji.. Ukiona wakosoaji unaona kama wamekosea wewe ndio upo sahihi.
Ikiwa wewe ni mtu wa kusifia sana utawala na unaona mazuri ya utawala ni mengi kuliko madhaifu usikasirike kuona wanaokosoa. Na ikiwa wewe ni mtu wa kukosoa usikasirike kuona wenzio wanasifia.
Suala la muhimu ni kwamba fanyeni yote kwa maslahi ya taifa. Kama wewe ni "Accorder" basi sifia sana.. sifia kwa nguvu zote.. Na kama wewe ni "Dissenter" kosoa sana.. kosoa kila unapoona kasoro.. Ili mradi wote mnafanya hayo kwa maslahi ya TAIFA.
Ukiona kundi moja kati ya "Accorders" na "Disentors" limelalamikia kundi jingine basi ujue kundi linalolalamika limeshindwa kwa hoja. Vijana wanasema "limeshikwa pabaya". Kama ni mgonjwa basi yupo ICU.!
Yani ukiona Mkosoaji (Dissenter) analalamika kwanini watu wanasifia tu ujue kwisha kazi. Na ukiona Msifiaji (Accorder) analalamika kwanini watu wanakosoa tu hawasifii hata kidogo ujue ameanza kukata tamaa.
Nimelazimika kutoa ufafanuzi huu baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa rafiki zangu wa chama chakavu. Mmoja ni amenitext akiniambia "hivi ndugu yangu huoni mazuri ya serikali hata moja?"
Jibu ni kwamba mazuri yanaweza kuwepo lakini si kazi yangu kuyaainisha, hiyo ni kazi yenu. Mimi kazi yangu ni kukosoa utawala ili ufanye mazuri zaidi kwa maslahi ya wananchi. Ukiona siku nimesifia ujue nimeamua kuwapa backup.. Yani kama ni soka nimeshakufunga 5-0 hivyo naamua nijifunge moja ili nikupe backup usitoke uwanjani ukiwa na "magoli zero"
Kwa hiyo mnaoweza kusifia serikali ya JPM sifieni. Tumieni kila ushawishi kusifia. Msitukane wanaokosoa. Msikasirike. Nyie sifieni. Wanapoongeza nguvu ya kukosoa na nyie ongezeni nguvu zaidi katika kusifia. Lakini fanyeni hivyo kwa lengo la kujenga si kubomoa. Kosoeni au sifieni kwa maslahi ya taifa.
Bahati mbaya wasifiaji mnaonekana kukata tamaa. Badala ya kusifia mnaanza kulalamikia wenzenu wanaokosoa. Acheni kukata tamaa.. Kukata tamaa ni dhambi.. Najua mmezidiwa nguvu lakini endeleeni kusifia tu. Andikeni makala zenye ushawishi, fanyeni utafiti wekeni data mitandaoni mkisifia serikali yenu.
Yapo mengi sana ya kusifia lakini mmeyaacha mnabaki kulalamika tu. Sifieni makusanyo ya kodi, sifieni bomba la mafuta la Tanga to Kampala, sifieni kufutwa kwa sherehe za Muungano... Mbona zipo agenda nyingi hamtaki kusifia badala yake mnalalamika tu??
Eti hivi Malisa haoni mazuri ya serikali? Anakosoa tu.. Hahaah naweza kuona mazuri lakini si kazi yangu kuyaelezea.. hiyo ni kazi yenu. Mbona hamtaki kutimiza wajibu wenu? Mnataka niwasaidie kusifia, mbona hamjawahi kunisaidia kukosoa??
Kazi yangu ni kuona kasoro na kuielezea ili serikali irekebishe kasoro hiyo na watanzania wapate nafuu ya maisha.
Kwa mfano kama kuna mfumko wa bei wananchi wananunua bidhaa bei ghali.. kazi yangu ni kukosoa na kuonesha "alternatives" ambazo serikali inaweza kuzitumia kupunguza mfumuko wa bei. Serikali ikitumia "alternatives" hizo na mfumuko wa bei ukapungua, watu wakapata unafuu wa maisha hiyo ndiyo furaha yangu.
Sasa wewe unataka nisifie tu..? Mbona wewe umeshindwa kusifia unabaki kulalamika? mtu mmoja alicomment kwenye post yangu moja kuwa namchukia Malisa anakosoa kila kitu. Lakini cha ajabu kila siku lazima apite kwny ukurasa wangu ajue nimeandika nini. Unawezaje kumchukia mtu ambaye unapoteza bundle yako kumsoma kila siku?
Huna haja ya kunichukia kwa sababu nakosoa serikali. Kama ww unataka kusifia just do it. Be smart.. play your part. Kumbuka kuna kundi kubwa sana la "Latent people" ambao hawataki kusifia wala kukosoa. Wanasubiri washawishiwe kwa hoja ili waunge mkono kundi mojawapo kati ya "Accorders" na "Dissenters"..
Sasa wewe badala ya kujenga hoja ili uwashawishi hawa "Latents" unabaki kulalamika.? Matokeo yake wakati "Accorders" mkilalamika, "Dissenters" wanajenga hoja zenye mashiko na kufanikiwa kushawishi "Latents" wengi.
Kwa hiyo kundi la "Dissenters" linazidi kujiongezea wafuasi kila siku, huku "Accorders" wakibaki kulalamika tu.
Msipokua makini mtaishia kulalamika tu na mkija kushtuka hata wale wasifiaji wenzenu mliokua nao mtakuta wameshawishiwa kwa hoja na washageuka kuwa wakosoaji. Kutahahamaki uchaguzi huo #2020.
NB:
Hii ni shule ya bure kwa wafuasi wa chama chakavu.. nimeona niwape shule bila ada maana wengi wenu ni wavivu wa kutafiti.. mnaweza kuitumia elimu hii au kuipuuza..
#ElimuElimuElimu.!
Malisa GJ.!