JOANNA
Senior Member
- Nov 1, 2010
- 112
- 355
Nchi haiwezi kuongozwa bila kufuata sheria na katiba ya nchi.Uongozi bora ni lazima uheshimu sheria za nchi na misingi ya haki. Kilichotokea Oktoba ni serikali kuvunja na kuidharau katiba ya nchi kwa kuwauwa wananchi wake.Hali hii imepelekea wananchi kutokuwa na uhakika wa usalama wao.
Swala la serikali kuruhusu watu wasio na sare(uniform) kubeba silaha za moto hadharani na kuuwa watu ni kosa kubwa sana la kiusalama kuwahi kutokea Tanzania.Kama ingekuwa ni nchi zenye kuruhusu raia wake kuwa na bunduki kama Marekani, kuja nyumbani kwa mtu na bunduki na huna uniform , raia wa nchi hizi wanahaki ya kujilinda kwa kutumia bunduki zao.
Ni kinyume cha sheria kuwaruhusu watu wasio na uniform, kitambulisho au badge kubeba silaha za moto hadharani nakuuwa watu, this violates gun laws.Sasa sababu wananchi walivyotoa zile picha mitandaoni na kusema hawa ndio waliowauwa ndugu zetu hamjajibu chochote.Hatujawaona mkikemea mauaji, hatujaona mkiwakemea wale wasio na uniform na kubeba silaha na kuwauwa watu, ndio maana huko mitandaoni sasa Gen Z nao wanazitafuta silaha kwa nguvu zote kwasababu wamegundua hawahitaji uniform kubeba silaha hilo mmewafundisha.Hili kosa tayari linawagharimu sasa hivi.
Mmeanza kuleta taarifa za kukamata mabomu kutoka kwa wageni, lakini mnasahau kuna raia waliwaletea taarifa na kuwaonya kwamba baadhi ya wauwaji hawakuwa raia wa Tanzania ila mkadharau.Sasa Gen Z nao wanatafuta misaada kusikojulikana. Kama mkichanganua mtagundua yale makosa ya kiusalama na uvunjwaji wa sheria mliyoyafanya ndio wananchi wanayafanya sasa.Raia wamegundua hakuna haki ya utekelezaji wa sheria hivyo wanatafuta mbinu nyingine za kujilinda.
Mpaka sasa polisi mmepoteza heshima na uwaminifu mliokuwa nao kutoka kwa wananchi.Mauaji ya wenye haki huleta uchungu na chuki. Wananchi hawana Imani na vyombo vya usalama.Yaani kweli raia anakuomba msaada ili umlinde unamuua, usaliti huu unasikitisha sana.Ukweli ni kwamba hamuwezi kuwaongoza raia kama raia hawatawapa kibali na ushirikiano wa kuwaongoza.
Serikali mkubali tu kwamba mpaka sasa mmeliweka taifa hatarini kwa kuvunja sheria nyingi sana.Je serikali ipo juu ya sheria. Sheria tunatakiwa tuziheshimu wote lakini nyinyi mmezivunja na sasa mnatulazimisha sisi tuzitii na kuziheshimu ili kuleta amani. How is that possible?Itawezekanaje pasipo nyie kuwajibika?Tunaka sheria hizohizo mnazotusisitiza nazo nanyie mzitekeleze.
Wasikilizeni wananchi,Serikali ni kwa ajili ya wananchi.Tukubaliane kwa uwazi, misingi ya haki ya uchaguzi haikufuatwa ,uchaguzi ni batili, huu ni uongozi wa mtutu wa bunduki. Serikali inapaswa kuwa ya watu kwa ajili ya watu, na si kwa ajili ya mtu na matakwa binafsi.
Zaidi ya watu elfu saba wanasadikiwa wameuwawa.Katika hili haki za kisheria zifuate na waliohusika wapelekwe mahakamani na ndipo tutaweza kuzungumza namna ya kujenga misingi ya haki tena ndani ya taifa letu.