Nathason2
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 598
- 680
Wapendwa wana JF
Naamini wengi wetu tunauelewa na hali ya jiji letu la dar es salaam kwa sasa, Hasai kwenye nyanja ya uchumi,hali ya maisha kwa vijana wengi sana mitaani imekuwa ngumu hususani wale waliokuwa wanaendesha maisha kiujanjaujanja hali hii imeongeza kundi la vibaka hivyo kupelekea kushamiri kwa vitendo vya uhalifu pamoja na wizi,leo mimi nimeona ni vyema tukakumbushana mambo kadhaa ambayo yanaweza kutuamsha na kutuongezea umakini.
Suala la kuhama nyumba/Makazi pia ni suala la kawaida watu wanahama kutoka Nyumba moja kwenda nyumba nyingine kutoka mtaa huu kwenda mtaa ule hii ni hali ya kawaida, hivo basi wapendwa mnashauriwa kuchukua tahadhari ya kutosha pindi unapo hamia nyumba nyingine/chumba kingine tambua kuwa huenda wewe ukawa sio mtu wa kwanza kuishi kwenye nyumba hiyo wako wengi wameishi hapo na pengine wanafunguo za mahali hapo hivo ni vyema kabla haujaanza maisha hapo ukakubaliana na mwenye nyumba yako akakubadilishia kitasa cha mlango,kwa sababu huwezi kujua ni watu wangapi wanafunguo za mlango/milango ya nyumba au chumba unachoishi
Usiwaachie Majirani zako funguo kwa sababu yoyote,wengi wetu tunajua jinsi uchongaji wa funguo ulivyo holela hapa mjini unaweza kumwachia jirani yako funguo hii leo then akachonga funguo kama hiyo baada ya kitambo kidogo akatumia funguo hizo kukuibia.
Imarisha ulinzi wa mali na nyumba yako kwa kadri ya kipato chako,uwezo wako na kwa kadri mazingira yanayokuzunguka yanavyoruhusu kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba Laptop,simu,Tv,friji ni vitu vidogoo lakini ukiibiwa vitakurudisha nyumba vitakufanya usifikie malengo uliyojiwekea hivo ni vyema ukaimarisha ulinzi wa nyumba yako/makazi/chumba chako.