Kuketi kwa muda mrefu ni hatari kwa afya ya binadamu

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,723
Ulikua unafahamu kwamba kuketi kwa muda mrefu ni hatari kwa afya yako? unaambiwa binadamu wa kawaida kwa sasa anakaa kwa muda wa saa nane mpaka saa tisa kila siku akiwa kazini, kwenye gari au nyumbani.

Ukiongeza saa nyingine 7 za kulala, inamaanisha unatumia robo tu ya muda wako ukiwa umesimama au ukiwa unatembea kwa siku ambapo muda huo mfupi wa kutuliza mwili unazidisha hatari ya unene lakini pia orodha ya maradhi mengine kama matatizo ya moyo, kisukari, saratani, magonjwa ya misuli, mgongo, mshtuko n.k

Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, Wanasayansi wanafananisha kukaa kama uvutaji wa sigara, ni kama mrundiko wa magonjwa ambayo hujionesha ukubwani.

Shirika la afya duniani limegundua kwamba kukaa bila kufanya kitu chochote ni chanzo cha nne kinachoua watu kwa kasi zaidi duniani ambapo pia ukiachana na kuongeza unene katika mwili imekua ikigharimu uchumi wa nchi ya Uingereza bilioni 145 kila mwaka kutokana na matatizo ya mgongo na misuli.

Shirika la afya duniani linashauri angalau kwa wiki mtu afanye mazoezi kwa dakika 150 ambazo ni sawa na saa mbili na dakika 40 ambapo ushauri mwingine ni wa labda dakika 30 kwenye siku tano, hiyo ni angalau kuliko kutumia muda mwingi kuketi ambako ni hatari kwa afya.
 
ngoja niuze gari fastaaa nirudie kudandia dala dala kama zamani mweee :majani7:

na ahsante kwa taarifa muhimu kama hii..
 
Hili unalolisema ni kweli kabisa lakini % kubwa hawawezi kukwepa hili labda msemo wa jamaa hapo juu kuwa wapiga debe, wamachinga ila wale wanaotembea, wauzaji wa vitu kwenye magari stendi n.k
 
Ni kweli mkuu mleta mada, ndio maana hata unapokuwa hewani kwenye safari ndefu inatakiwa unyanyuke japo utembee tembee kwenye uwazi
 
Waondoe viti maofisini na kwenye nyumba za ibada.
Ulikua unafahamu kwamba kuketi kwa muda mrefu ni hatari kwa afya yako? unaambiwa binadamu wa kawaida kwa sasa anakaa kwa muda wa saa nane mpaka saa tisa kila siku akiwa kazini, kwenye gari au nyumbani.

Ukiongeza saa nyingine 7 za kulala, inamaanisha unatumia robo tu ya muda wako ukiwa umesimama au ukiwa unatembea kwa siku ambapo muda huo mfupi wa kutuliza mwili unazidisha hatari ya unene lakini pia orodha ya maradhi mengine kama matatizo ya moyo, kisukari, saratani, magonjwa ya misuli, mgongo, mshtuko n.k

Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, Wanasayansi wanafananisha kukaa kama uvutaji wa sigara, ni kama mrundiko wa magonjwa ambayo hujionesha ukubwani.

Shirika la afya duniani limegundua kwamba kukaa bila kufanya kitu chochote ni chanzo cha nne kinachoua watu kwa kasi zaidi duniani ambapo pia ukiachana na kuongeza unene katika mwili imekua ikigharimu uchumi wa nchi ya Uingereza bilioni 145 kila mwaka kutokana na matatizo ya mgongo na misuli.

Shirika la afya duniani linashauri angalau kwa wiki mtu afanye mazoezi kwa dakika 150 ambazo ni sawa na saa mbili na dakika 40 ambapo ushauri mwingine ni wa labda dakika 30 kwenye siku tano, hiyo ni angalau kuliko kutumia muda mwingi kuketi ambako ni hatari kwa afya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom