Asante mkuu kwa ushauri wakoNI RUHUSA KWAKO KUBADILI MAWAZO.
Kwa mfano umeshakubaliana na mtu mtafanya kitu fulani halafu dakika za mwisho anakuambia nimebadili mawazo, sitafanya tena kama nilivyokuambia. Unajisikiaje? Unachukuliaje hali kama hiyo?
Labda ni biashara na umeshakubaliana na mteja ila baadae anakuambia nimebadili mawazo. Au ni kwenye ajira na umeshakubaliana kitu fulani na mwajiri wako, umeshajiandaa kabisa na anakuambia nimebadili mawazo, hutafanya tena hivyo. Au ni kwenye maisha yako ya kawaida, ulipanga muoane na mtu na dakika za mwisho anakuambia nimebadili mawazo? Au umeshaona na mtu na kati kati ya safari anakuambia nimebadili mawazo?
Najua kama wewe ndio umeambiwa hivi unaweza kujisikia vibaya sana. Unaweza kuona aliyebadili mawazo hafai na ameharibu maisha yako. Lakini ukweli ni kwamba yeye ametumia haki yake ya msingi, kuruhusu mawazo yake yamchagulie kile ambacho anaona ni bora kwake. Hakuna jinsi unaweza kuzuia hilo.
Badala ya wewe kulalamika kwamba kwa nini hakukwambia mapema au kwa nini alikubali mwanzoni, furahi kwamba umejua mapema kabla hata hujapoteza muda mwingi. Shukuru kwamba umejua ni mtu wa aina gani na jifunze wakati mwingine kuangalia vitu muhimu kabla hujaingia kwenye makubaliano na mtu ambayo ni muhimu.
Jipe ruhusa ya kubadili mawazo, wape wengine ruhusa ya kubadili mawazo na usitake kuishi maisha ya kufungwa au kuwafunga wengine kwa sababu tu wanaogopa kubadili mawazo. Maisha yanapaswa kufurahiwa na sio kuishi kwa ajili ya kuwaridhisha wengine.
TAMKO LA LEO;
Najua nina ruhusa ya kubadili mawazo hata kama nilishakubaliana na mtu. Najua pia kwamba watu wana ruhusa ya kubadili mawazo yao hata kama walishaniahidi kitu. Naheshimu uhuru wangu na wa kila mtu na ni kwa uhuru huu ndio naweza kuishi maisha ninayoyafurahia na yenye faida kwa wengine pia.
chalii wa ara Muwe na siku Njema
Karibia wote.......
Hapo kumbuka sijaadd hirizi la mjepu...........
Ni binti tuliojuana naye kwa muda wa kama miezi minne sasa, tulianza kufahamiana kupitia WhatsApp, tukachat muda mrefu mpaka kufikia kuwa wapenzi, japo tulikuwa mikoa ya mbali.
Tulitumiana picha na videos na kujuliana hali muda wote, basi tu ili tuzidi kuwa karibu japo hatukuwahi kuonana uso kwa uso! Leo ni siku ambayo sitoisahau maishani, mwangu! Nimefunga safari ya kuja kuonana nae, tulikutana na binti muda wa kama masaa mawili hivi, tukatembea na kuzungumza pamoja huku kila mmoja wetu akiwa mchangamfu kwa mwenzake.
Nilimuandalia na zawadi ndogo tu nikampa. Mida ya jioni ilipofika tuliachana na kila mmoja kuelekea nyumbani anakoishi. Nimefika nyumbani, nakuta message ya yule binti kwenye simu yangu ikisema "Samahani, moyo wangu umeshindwa kukupenda, naomba unisamehe".
Ilibidi nimpigie simu muda ule ule kumuuliza kwanini, lakini hakunipa jibu, aliniambiya tu hata yeye hajui moyo tu umekataa. Roho imeniuma sana. Najiuliza mpaka sasa ni nini alichotaka kuona kutoka kwangu, kama ni hali ya maisha nilimuelzea ukweli kitambo, muonekano wangu, ongea yangu vyote anavijua!
Roho inaniuma sana. Nimeshindwa kwakweli kukaa nalo moyoni nikaona nililete huku kwenu kwa ushauri.
Wadau, tatizo itakuwa nini? Au mnanishauri nini juu ya hili? Maana nipo njia panda.
Usisahau kuna kunuka midomo etc ambayo si rahisi kujua kwa kuchati au kupiga simuSijui amepatwa na nini,ila pole. Kubali tu matokeo japo sio rahisi,ila huwezi kulazimisha maji kupanda mlima. Jiweke pembeni subiri wa kwako
huh !!! :shock: :A S confused::A S-confused1:Uwiiiiiiii............umenifika hapa...........
Usisahau kuna kunuka midomo etc ambayo si rahisi kujua kwa kuchati au kupiga simu
Mbona kama ulipendeza tu.......labda hizo raba zilikuwaje.....?.....isije kuwa zile ulimi nje.......au mkate boflo........unajua swala la viatu wadada tunaangalia sana.........
Lakini kwa maelezo yako.......nadhani ulipendeza........dada tu anataka kukuletea tashtiti......we kutana nae hiyo jumamosi.......halafu uje utuambie kasemaje.........
Usisahau kunitag........sawa eeeh.......
Labda hajavutiwa na wewe baada ya kukuona. Au maybe jinsi mazungumzo yenu yalivyokuwa, na jinsi alivyoobserve baadhi ya Vitu vyako, akajikuta moyo wake umekukataa.
Blind dates zina challenges pia haswa inapotokea mnakutana afu wewe ndo ukakolea while mwenzako akakukinai. Sio issue lakini, shukuru tu Mungu dada wa watu kawa honest na wewe, hajataka kukupa matumaini wala kukupotezea muda. Shukuru kwa yote, jikaze maisha yaendelee.
Si kwamba labda ananijaribu pengine!!Tumepanga kukutana nae jumamosi ngoja nikamsikilize!!ka vp napiga chini siwezi kulazimisha kupenda pasipopendeka
Hapana mkuu wala ckujikweza nilikuwa kawaida tu japo tulikuwa tunazungumza huku tukiwa tunatembea kumsindikiza kwao!!Kwa kifupi hatukupata mda wa kuzungumza alikuwa na haraka!Nimeshindwa kumuelewa hata hajanijua vizuri kafikia uamuzi huoHukujikweza kweli kaka???