Kukaribia bila ya kufika kwa upinzani nchini.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukaribia bila ya kufika kwa upinzani nchini..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Nov 24, 2011.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kukua kwa upinzani nchini haswa baada ya chaguzi ya taifa ya 2010, bado inavyoonekana kuna kusita sita kwa watanzania wengi katika kuwapa na kuwaongezea wapinzani nguvu ili kuleta changamoto ya ukweli ya kiuongozi nchini...

  Hii ni pamoja na kashfa, uongozi mbovu, na kuendelea na kuongezeka kwa kero nyingi za kijamii, kiuongozi na kiuchumi katika mamlaka ya serikali ya CCM.

  sijaweza kuona bado wimbi au kiwungu nilichokitegemea cha mabadiliko ya taswira na ari ya wananchi katika kuiondoa CCM kuelekea chaguzi muhimu ya 2015,(kiwingu cha expected voters backlash against CCM kama ilivyokuwa Zambia 2011 hakipo kabisa) Na hili limenifanya kufikiria kuwa tatizo liko kwenye vyama vya upinzani vyenyewe na taswira hasi iliyojijenga kwa miaka mingi kuhusu vyama hivi na inaonekana mpaka pale wanaCCM "wazuri" ,(kama Dr SLaa) watakapotoka CCM na kuanzisha chama chao au kujiunga na upinzani ndiyo upinzani utakuwa na sauti na kushinda uaminifu wa bila kusita wa watanzania wote..

  Mifano hai tena nchi jirani ipo (bila ya KANU kumegeka na kumsapoti Kibaki KANU isisngeshindwa 2002 na Michael Sata ameingia kwa sababu alijitoa MMD kuunda chama chake sasa hawa viongozi wa CCM wasiothaminiwa na mfumo huu wa kifisadi wa CCM wanasubiri nini? Si muasisi wa CCM Mwl Nyerere alishawapa taa ya kijani ya kuondoka na kuupa nguvu upinzani kwa kusema kwamba upinzani wa kweli utatoka CCM?
   
Loading...