Kujiuzulu kwa kumuunga mkono Rais

Kujiuzulu kwa kumuunga mkono Rais

apolycaripto

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Posts
644
Reaction score
225
Ufuasi wa siasa katika vyama hujengwa katika misingi ya itikadi. Swali la kujiuliza ni Je, wanaojiuzulu kwa kumuunga mkono rais kisha wanaenda kuchukua kadi za chama (ambacho kinaongozwa katika misingi ya itikadi) ni sahihi?

Hivi huyu Rais atakapomaliza muda wake, hawa watu watamuunga mkono nani?

Nakiona chama A kinaelekea kufanya makosa yaleyale ambayo yanakisumbua chama B.

Kwa sisi ambao tumekuwa tukipambana chama A, tunaposhindwa katika kura za maoni, imekuwa rahisi sana kushawishiwa kwamba ingia chama B utapita kwa urahisi. Kweli matokeo chanya tumeyaona lakini kwa upepo huo huo chama B kinapukutika. Hivi hii haiwezi kuleta mpasuko kwa chama A katika nyakati za usoni?

Ni dhahiri kuwa wimbi hili la sasa limechagizwa na ahadi za vyeo, kupewa fursa ya kutetea nafasi ile ile. Vipi mambo yakiwa tofauti?

Naziona nyakati mbaya za chama A kwa siku za usoni kama chama B kinavyotaabika sasa.

Siasa ni sayansi, through experiment we can get a better solution.
 
Achaa kufukutaa moto kwa bdole vyakoo. Watu waogaa waogaa hatuwatakii humu jamvin. Semaa ccm kwendaa chadmaa au chdmaa kwndaa ccm au nccr
 
ccm ina pesa inawalip makada
njaa ni mbaya sio nzuri
CCM ukijulikana wewe ni chama pinzani unaandamwa mpaka unaweza haribia biashara zako zote hii ndio silaha ccm wanayotumia ila siku hii silaha ikiisha makali ccm itapukutika kama mbuyu wakati wa kiangazi
 
Back
Top Bottom