Kujitenga na Siasa ni Kufanya Siasa

Sci-Fi

Member
Joined
Jan 30, 2016
Posts
74
Reaction score
275
Habarini wanaJF, mara kadhaa nimekua nikijiuliza. Hivi kweli inawezekana mtu akaamua kabisa kabisa kijitenga na siasa??

Nimekuja gundua kwamba, kwa hali ya kawaida kabisa, "hapana", haiwezekani mtu kujitenga na siasa, kwa sababu siasa ndiyo inaunda mfumo unaogusa kila kipengele cha maisha ya mwanadamu, iwe unataka au hutaki.

Hizi hapa sababu kuu;
  1. Siasa inaunda sheria tunazoishi chini yake.
Kila kitu tunachofanya, kuendesha gari, biashara, kuoa, kusoma, kumiliki mali, hata kuchangia kanisani/msikitini, kinaongozwa na sheria zilizotungwa na wanasiasa. Na hatuwezi kuziepuka.

2. Siasa inaamua uchumi unaotuathiri
  • Bei ya mafuta
  • Kodi tunazolipa
  • Ajira na mishahara
  • Bei ya vyakula
  • Mfumuko wa bei
Vyote hivi haviamuliwi na malaika, vinaamuliwa na maamuzi ya kisiasa.
Hivyo mtu anaweza kutaka “kutotaka siasa”, lakini uchumi unamlazimisha kuingia kwenye siasa.

3. Siasa inaamua huduma tunazopata
  • Afya ikoje
  • Elimu ya watoto wako ikoje (wakiwekwa wanasiasa vilaza ukiamua hatma ya Elimu ya Taifa shida kubwa inakwenda kutokea)
  • Maji na umeme vinapatikana
  • Barabara zinajengwa?
Huduma hizi zinapatikana kulingana na vipaumbele vya serikali, ambavyo ni maamuzi ya kisiasa. Hakuna njia ya kuishi nje ya haya. Hivyo mnadai kwamba hamtaki kujihusisha na siasa jitafakarini mnacho kikataa.

4. Siasa inaamua utu wako na haki zako. Haki zako kama;
  • Uhuru wa kuongea
  • Uhuru wa kuabudu
  • Haki ya kuishi
  • Haki ya kupiga kura
Vyote hivi viko mikononi mwa mifumo ya kisiasa. Ukikaa kimya, bado unagusa haki hizi, kwa sababu tafsiri ya haki kwa wananchi hupewa na wanasiasa waliopo madarakani. Angalia kinachoendelea Tanzania. Juzi tu hapa Wanasiasa kupitia Polisi walitanga tuanE kulala/kukaa ndani na ikawa. Sasa endelea kusema hujihusishi na siasa.

5. Kutofanya siasa pia ni kufanya siasa. Kama huongei kuhusu siasa:
  • Unaipa nafasi dhuluma kukua (unakua chawa ambaye haoni maovu bali mazuri tu ya boss wake, hivyo haki inaanza kutafsiriwa kwa namna apendavyo boss)
  • Unaruhusu maamuzi kufanywa bila ushiriki wako
  • Unaruhusu ubaya kushinda wema
Katika maisha, mtu mkimya ni ushindi wa walio na nia mbaya. Hata kusema "sitaki siasa" ni msimamo wa kisiasa, kwa sababu unaathiri matokeo ya kisiasa.

6. Biblia inathibitisha kuwa kujitenga na mamlaka si wito wa Mungu

Katika Biblia: Manabii walikemea wafalme (Eliya, Isaya, Nathani, Yohana Mbatizaji). Yesu mwenyewe alizungumzia haki, dhuluma, uongozi, kodi na serikali. Kanisa la kwanza lilitetea haki za waumini mbele ya watawala. Hata Mungu mwenyewe aliweka mfalme, sheria na mahakama katika Israeli. Hivyo siasa si kitu cha shetani, ni mamlaka ya kuongoza wanadamu, na inapoharibika, watu wa Mungu hawapaswi kukaa kimya.

Kwa nini watu wengine hudai “tuachane na siasa”? Wanasiasa huwa wanasema tusichanganye dini na siasa.

Sababu zao mara nyingi ni:
  1. Kutaka kudhibiti watu ili wasipaze sauti. Kama yanayoendelea Tanzania.
  2. Hofu ya kukosolewa
  3. Kutaka kutumia dini kwa maslahi bila kuchungwa
  4. Kutotaka kuwajibishwa
Jambo la kusikitisha katika nchi yangu hii, ni kwamba, viongozi wa dini wakizungumza siasa → “wanavuka mipaka”. Lakini viongozi wa serikali wakizungumza siasa kwenye nyumba za ibada → “wanazungumza na wananchi.” Tusiache kuzungumza siasa hata kama wanakereka. Ukweli ni kwamba: Siasa ni kama hewa, huwezi kuikwepa. Unaweza tu kuamua kuipumua kwa hekima au kuiachia ikudhibiti. Haiwezekani kujitenga na siasa. Inawezekana tu kuwa mkimya ndani ya siasa, lakini si kuiepuka.

Kamwe tusichoke kuipigania nchi yetu kwa kufanya siasa safi ikiwa ni pamoja na kudai mambo yote ya Msingi kwa hatma njema ya vizazi vyete;
  1. Katiba Mpya
  2. Tume Huru ya Uchaguzi.
  3. Uwajibikaji na Uwajibishwaji..n.k.
 
Kila mmoja na fikra zake usitujumuishe. Wewe unataka katiba mpya, tume huru, mm sitaki kwasasababu sijaona shida na katiba mliyopo, mtaniambiaje nifanye siasa!?.

Waliopo sijaona kosa lao kwanini nijihusishe!?.
Kufata amri ya waliopo madarakani haimaanishi huwezi kuikwepa siasa, unakwepa siasa kwa kuacha wengine wajihusishe kwaniaba yako, hapo umeikwepa siasa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…